• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Wanamazingira warai Wakenya kupanda miti kutunza mazingira

Wanamazingira warai Wakenya kupanda miti kutunza mazingira

NA KENYA NEWS AGENCY

MWANAMAZINGIRA kutoka Kaunti ya Makueni, Evans Maneno amewarai Wakenya washiriki upanzi wa miti ili kutunza mazingira na kukabiliana na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Alisema kupitia upanzi wa miti, jamii itasaidia kupunguza athari ya kupanda kwa kiwango cha joto, ukame na kukauka kwa chemichemi za maji.

“Mnafaa kupanda miti kuzuia ukame, kukauka kwa chemichemi za maji na kupunguza athari ya uchafuzi wa mazingira,” akasema Bw Maneno.

Alikuwa akizungumza katika Taasisi ya Mafunzo ya Kimatibabu ya Mbuvo wakati wa kuadhimisha siku ya misitu ulimwenguni.

Wakati wa maadhimisho hayo, miche 200 ilipandwa huku mingine 800 ikitarajiwa kupandwa kati ya Machi- Aprili.

  • Tags

You can share this post!

Kivumbi cha udiwani cha Ichagaki chavua...

Kocha wa Leads United akiri kuponea chupu kwa ushindi...

T L