• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Wasafiri 7 kutoka Tz waponea baada ya boti lao kuzama

Wasafiri 7 kutoka Tz waponea baada ya boti lao kuzama

Na KALUME KAZUNGU

MABAHARIA saba kutoka Tanzania waliponea chupuchupu, boti lao liliposombwa na mawimbi makali na kuzama kwenye bahari Hindi katika eneo la Shanga, Kaunti ya Lamu.

Ilibainika kuwa saba hao walikuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam, Tanzania, kuelekea Kismayu nchini Somalia kuchukua mzigo wa vyuma vikuukuu ajali hiyo ilipotokea.Walitambuliwa kama Swaleh Ramadhani Katambo, Mganga Mgoya, Abas Muharami, Msafiri Abdallah, Omari Jalala, Ibrahim Matoye Tumaini na Mohamed Salim.

Akithibitisha ajali hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Walinzi wa Baharini (KCGS), Bw Loonena Naisho, alisema kuwa maafisa wake kwa ushirikiano na wanajeshi wa majini, walifaulu kuwaokoa mabaharia hao wote wakiwa hai pamoja na mizigo yao.

Boti yao MV Al Feroz iliyozama baharini ilikuwa bado haijapatikana tukienda mitamboni.Bw Naisho aliwashauri watumiaji bahari kuwa waangalifu na kuepuka sehemu zinazojulikana kuwa na kina kirefu, hasa msimu huu ambapo bahari inashuhudia upepo na mawimbi makali.

“Tukitii maelekezo hayo tutaepuka ajali, maafa na mali kuangamizwa baharini,’ alieleza.Bw Katambo, ambaye ni msemaji wa mabaharia hao, alishukuru vitengo vyote vya usalama Kenya vilivyohusika katika shughuli hiyo ya uokoaji.

“Tuliwapigia simu na baada ya muda mfupi wakafika kutuokoa. Japo boti yetu ilizama twafurahia kuwa hai,” akasema Bw Katambo.Naye Bw Mgoya alishukuru uhusiano kati ya Kenya na Tanzania, akiutaja kuwa kichocheo kilichowezesha wao kupata usaidizi wa haraka.

walipokumbwa na tatizo baharini.Kamishna wa Kaunti ya Lamu, Bw Irungu Macharia pia aliahidi kwamba raia wa Tanzania waliookolewa watasaidiwa kurudi nchini kwao.

Bw Macharia aidha aliwashauri mabaharia kuzingatia maonyo yanayotolewa kuhusiana na hali ya hewa na bahari ili kuepuka kuendeleza safari baharini nyakati mbaya.

  • Tags

You can share this post!

Kocha aliyechagua kufunza uwanjani badala ya darasani

Ruto atumia tena Biblia kugonga Uhuru na Raila