• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Washukiwa wa ulaghai walemewa kulipa dhamana ya Sh8m

Washukiwa wa ulaghai walemewa kulipa dhamana ya Sh8m

Na RICHARD MUNGUTI 

WAKURUGENZI wawili walioghushi cheti cha ulipaji kodi ili kampuni yao ishinde zabuni ya kununua taa za kutumika wakati wa uchaguzi mkuu wa 2013 wameshindwa kulipa faini ya Sh8milioni waliyotozwa Jumanne.

Benson Gethi Wangui na Joyce Makena walitozwa faini ya Sh4milioni kila mmoja ama watumikie kifungo cha miaka mitano wakishindwa kuilipa.

Hakimu mkuu mahakama ya kuamua kesi za ufisadi alisema Gethi na Makena ndio walipanga njama ya kubadilishwa kwa hati za tenda waliyowasilishwa kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Hati hizo zilibadilishwa na mafisa wawili wa IEBC Kennedy Ochae na Gabriel Ngonyo Mutunga.

Mutunga alitozwa faini ya Sh2.8milioni naye Ochae akaagizwa alipe faini ya Sh200,000.

Mugambi alisema Ochae alikuwa na umri wa siku 21 tangu aajiriwe 2013 alipoghushi hati hizo za kampuni ya Solarmak Technologies Limited (STL) kuonyesha ilikuwa itumie Sh105milioni kununua taa hizo za kutumia miale ya jua kuwaka.

Aliyekuwa meneja wa shughuli za mauzo IEBC Willie Gachanja Kamanga,70, alitozwa faini ya Sh800,000 kwa kushindwa kulinda hati za zabuni za IEBC za kununua vifaa mbali mbali ambavyo vingelitumika wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Hakuna mmoja kati ya hao watano aliyeweza kulipa faini waliyotozwa.

Mugambi alisema amewatoza faini kwa vile  ni wakosaji wa mara ya kwanza.

“Tumepigana vita vilivyo vyema tangu 2013 lakini tumefikia ukingoni sasa haki itatwaa usukani,” wakili Paul Kamau aliyewatetea washtakiwa walioghushi zabuni ya ununuzi wat aa za kutumika wakati wa uchaguzi mkuu wa 2013.

Licha ya kupigana kufa na kupona  washtakiwa waliopatikana na hatia ya kughushi zabuni ya taa za kumulika wakati wa uchaguzi wa 2013 juhudi zao za kuachiliwa huru ziligonga mwamba na sasa watawasha hizo taa jela wakishindwa kulipa faini ya Sh11.8milioni ama watumikie kifungo cha miaka 16 gerezani

Ilibidi Bw Kamau anukuu kifungu cha II Timotheo 4:7 kumshawishi  hakimu mkuu mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Lawrence Mugambi awaonee huruma walaghai hao.

Hata hivyo Bw Mugambi alisema makosa waliyofanya washtakiwa Gethi, Makena, Mutunga, Kamanga na Ochae ni mabaya kwa vile tume huru ya uchaguzi na mipaka ingelipoteza Sh105milioni.

“IEBC ingelipoteza Sh105milioni kama zabuni hiyo haingelisimamishwa na Serikali,” alisema Bw Mugambi.

Hakimu huyo alisema sakata hiyo ilibuniwa na Gethi na Makena ambao ni wakurugenzi wa kampuni ya Solarmak Technologies Limited 2013.

Solarmak iliwasilisha ombi kwa IEBC ipewe tenda ya kununua taa za kutumia nishati ya jua kuangaza wakati wa kuhesabu kura wakati wa uchaguzi mkuu wa 2013.

Solarmak ilieleza IEBC itanunua taa hizo kwa bei ya Sh147milioni.

Lakini kampuni nyingine Konexion Limited iliyoomba zabuni hiyo pia ilikuwa imeeleza IEBC itanunua taa hizo kwa bei ya Sh107milioni.

Baada ya kupashwa habari  Konexion ilikuwa imetaja bei ya chini , Solarmak iliwatumia maafisa wa IEBC kubadilisha hati zake kuonyesha itazinunua taa hizo kwa bei ya Sh105milioni.

“Solarmak ndiyo ingelinufaika na ufisadi huo wa kubadilishiwa nakala za hati zake,” alisema Mugambi.

  • Tags

You can share this post!

Man-City watinga robo fainali za FA

Linturi aishtaki Serikali kufuatia kukamatwa kwake

T L