• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 5:06 PM
Wawili washtakiwa kujifanya wanahabari

Wawili washtakiwa kujifanya wanahabari

Na RICHARD MUNGUTI

WANAUME wawili walikamatwa wakijaribu kuingia katika bunge la Seneti wakijifanya kuwa wanahabari.

Wawili hao Thomas Ochieng Owino na Fred Odanga Azelwa walifunguliwa mashtaka Ijumaa katika mahakama ya milimani kwa kutoa habari za uwongo kwa afisa wa uhusiano katika bunge la Seneti (PRO) Bw James Macharia.

Walikabiliwa na shtaka la kujitambulisha kuwa wanachama wa baraza la wanahabari nchini MCK.Mabw Owino na Azelwa  walishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi katika mahakama ya Milimani Nairobi Bw David Ndungi.

Walikanusha mashtaka matatu ya kujitambulisha kuwa wanachama wa MCK, kughushi kadi ya MCK na kumkabidhi afisa wa umma kadi hiyo feki.Mabw Owino na Azelwa walikana walijitambua kwa Bw Macharia kuwa wanachama wa MCK wakiwa na lengo la kuingia katika jengo la KICC mnamo Julai 21, 2021.

Mahakama ilifahamishwa na kiongozi wa mashtaka Bw Abel Omariba kwamba watu hawaruhusiwi kuingia katika bunge la Seneti kiholela.Bw Omariba alisema Bw Azelwa alikutwa na kadi hiyo feki akiwa na lengo la kulaghai.

Mnamo Julai 9, 2021, Bw Azelwa alishtakiwa kumkabidhi Bw Macharia kadi hiyo akijua haikuwa halali.Washtakiwa waliomba waachiliwe kwa dhamana.Kila mmoja aliachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000 .

Kesi dhidi yao itatajwa Oktoba 8, 2021.

  • Tags

You can share this post!

Afisa ajipata taabani kwa kukejeli jaji

Upasuaji waonyesha daktari alikufa kwa sumu