• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Wawili wazuiliwa kwa mauaji

Wawili wazuiliwa kwa mauaji

Na RICHARD MUNGUTI

WASHUKIWA wawili wamezuiliwa kuhojiwa kwa mauaji ya  rafiki yao katika mtaa wa mabanda wa Kabarage eneo la Gigiri kaunti ya Nairobi.

Joseph Sila Mutunga na Josephat Njuguna Kung’u waliagizwa wazuiliwe kwa siku 4 kuhojiwa kuhusiana na kifo cha Wilson Ukiru.

Afisa anayechunguza kesi hiyo aliomba Konstebo Sheban Baraka alimweleza hakimu mkazi mahakama ya Milimani Bi Jane Kamau kwamba “anahitaji muda kuwahoji washukiwa hao.”

Wawili hao walikuwa wamekamatwa pamoja na mmiliki wa kilabu cha kuuza pombe Bi Agusta Kathomi Francis.

Konstebo Baraka alieleza mahakama kuwa mnamo Machi 28, 2021, Sila na Njuguna walimsindikiza Ukiru kuabiri gari inayoelekea mtaa wa Embakasi mwendo wa saa saba mchana.

Mahakama ilijulishwa hatimaye maiti ya Ukiru ilikutwa nje ya kilabu cha Kathomi ikiwa na majeraha.

“Naomba mud wa kuwahoji washtakiwa hawa pamoja na kuandikisha taarifa kutoka kwa mashahidi wengine,” alisema Konst Baraka.

Mahakama ilifahamishwa kuwa washukiwa hao wawili walikuwa wameabiri boda boda wakimsindikiza marehemu.

Konst Baraka pia aliomba mahakama imwachilie Kathomi kwa vile “ni shahidi wa serikali katika mauaji hayo.”

Mahakama iliamuru kesi hiyo itajwe Aprili 12, 2021 ndipo ujumbe uwasilishwe ikiwa uchunguzi umekamilishwa.

“Kesi dhidi yako imeondolewa,” hakimu alimweleza kathomi.

Mahakama ilimweleza mshukiwa huyo kwamba “atageuzwa kuwa serikali katika kesi hii ya mauaji.”

  • Tags

You can share this post!

Mwanaharakati taabani kwa kutania Rais

Ubakaji: Mahakama yanyima 2 dhamana