• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 6:55 PM
Weledi wa demu wangu chumbani umenitia wasiwasi

Weledi wa demu wangu chumbani umenitia wasiwasi

SHANGAZI;

Kuna jambo limefanya nianze kumshuku mwanamke mpenzi wangu. Ustadi wake chumbani hauna mwingine. Kila tukikutana anakuja na mtindo tofauti. Nina wasiwasi.

Mwanamke akimpenda mwanamume anaweza kufanya chochote ili kumfurahisha. Huna sababu ya kumshuku. Ninaamini anajitahidi tu kukupa raha na kudumisha uhusiano wenu.

Kumbe niliyeingiza boksi ni tapeli wa mapenzi!

Kuna mwanamke nilimfungulia moyo wangu miezi miwili iliyopita na akakubali. Juzi alinitumia ujumbe kuniambia niachane naye kwani ni mke wa mtu. Nimemsaidia sana kwa pesa nikiamini atakuwa wangu.

Mwanamke huyo ni tapeli wa kimapenzi. Nia yake ilikuwa kukunyonya pesa ndiposa alikubali ombi lako mara moja. Labda hata si mke wa mtu. Itabidi tu uachane naye utafute wa kweli.

Mama ya mpenzi wangu amenitupia chambo!

Nimejua kwa nini mama ya mpenzi amekuwa mkarimu sana kwangu tangu tujuane. Juzi alinitumia ujumbe eti ananipenda na kuomba niachane na binti yake ili tuwe wapenzi. Hajaolewa na bado ni mrembo. Nishauri.

Mapenzi ni chaguo la mtu. Pili, kipendacho moyo ni dawa. Mama ya mpenzi wako ameungama mwenyewe kwamba anakupenda. Sasa itabidi uamue kati ya kuku na yai lake. Kazi kwako.

Boi ametisha kuniacha nisipomwonjesha tunda

Mpenzi wangu amekuwa akitaka kuonja asali lakini nimekataa kwa sababu siko tayari. Sasa anatishia kuniacha na sijui nitafanya nini kwa sababu nampenda sana.

Kuna masharti yasiyowezekana katika uhusiano wa kimapenzi. Kama mpenzi wako ameamua ni lazima aonje asali la sivyo akuache, hiyo ina maana hakupendi, anaongozwa na tamaa. Achana naye, utapata mwingine.

  • Tags

You can share this post!

Nyaribo kusalia gavana baada ya kura ya kumng’atua...

Ifahamu ngoma maalumu ya kujivunia ubikira wa wanawake wa...

T L