• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Wito mwongozo maalum wa akili mwigo AI utumike kufanikisha maendeleo barani

Wito mwongozo maalum wa akili mwigo AI utumike kufanikisha maendeleo barani

NA LAWRENCE ONGARO

WATAALAMU wa sekta za umma na za kibinafsi barani Afrika wamehimizwa kubuni na kukumbatia matumizi ya teknolojia ya kuiga akili ya binadamu  (Artificial Intelligence – AI) kwa ustawi na maendeleo.

Hayo yalijadiliwa na wataalamu wa teknolojia wa Microsoft Africa Research Institute (MARI) kwenye kongamano kuhusu mjadala huo.

Kongamano hilo la siku moja jijini Nairobi lilitoa pendekezo jinsi wataalamu wanavyostahili kubuni ujuzi huo wa muigo wa akili ( Al) utakaoweza kuambatana  na teknolojia ya kisasa.

Akizungumza katika kongamano hilo, mkurugenzi wa Mari Dkt Jacki O’ Neill alisema ubunifu huo wa AI utasaidia kubadilisha maswala mengi barani Afrika.

“Tutaona mabadiliko kadha iwapo tutatilia maanani ubunifu huo wa akili kupitia teknolojia,” alisema Dkt O’ Neill.

Alisema iwapo mwongozo huo utatekelezwa katika sekta tofauti barani Afrika, bila shaka changamoto nyingi zitapunguzwa kwa kiwango kikubwa.

Aidha alisema hiyo ni nafasi njema kwa wataalamu kutoka kila sekta kuwasilisha maoni yao kujadili maswala hayo ya kidijitali kwa lengo la kupata mwelekeo wa kuboresha biashara barani Afrika.

Baadhi ya nchi za bara Afrika ambazo zinalenga kuhusishwa na ubunifu huo ni Misri, Mauritius, na Tunisia.

Akizungumza katika hafla hiyo, mkurugenzi katika shirika la Future Research Stellenbosch Business School, Dkt Njeri Mwagiru alisema ni vyema washikadau wote wajitokeze mhanga kufanikisha ubunifu huo utakaoleta mabadiliko katika sekta ya ukuaji wa kiteknolojia.

Mpango huo unatarajiwa kushika mizizi katika bara la Afrika kutokana na jinsi biashara tofauti zinavyopanuka kupitia teknolojia.

Kongamano hilo liliwaleta pamoja washika dau wa kibinafsi na umma kutoka bara lote la Afrika huku kila mtaalamu akihimizwa kuonyesha ujuzi wake.

Anaeleza kwamba Microsoft imebadilisha  maswala mengi katika maeneo mengi ulimwenguni.
  • Tags

You can share this post!

Jamii Lamu yaahidi kusaidia serikali kutokomeza Al-Shabaab

Ex wa Bahati, Yvette Obura ‘aringisha’ kadudu...

T L