• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 7:50 AM
Zaidi ya hospitali 17 za umma kuzinduliwa Nairobi

Zaidi ya hospitali 17 za umma kuzinduliwa Nairobi

Na SAMMY WAWERU

HUDUMA za afya katika Kaunti ya Nairobi zinatarajiwa kuimarika kufuatia ujenzi wa zaidi ya hospitalini 17 unaoendelea.

Rais Kenyatta ametangaza kwamba hivi karibuni atazindua rasmi utendakazi wa vituo saba vya afya.

“Miezi mitatu baadaye nitazindua hospitali zingine, zaidi ya 10. Lengo langu ni kila mwananchi apate huduma bora na kwa bei nafuu,” akasema Rais.

Ujenzi wa vituo hivyo vya afya unaendeshwa na Shirika la Kuimarisha na Kustawisha Huduma za Jiji la Nairobi (NMS) chini ya uongozi wa mwenyekiti wake, Meja Jenerali Mohammed Badi, na Rais Kenyatta amesema shughuli hiyo inalenga kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, KNH.

Chini ya mojawapo ya Ajenda zake Nne Kuu, matibabu bora na ya bei nafuu, Rais Kenyatta alisema lengo lake ni kuona gharama ya matibabu imerudi chini.

“Tunataka huduma za matibabu ambapo familia haitalemewa mmoja wa wanafamilia anapougua. Tumeona baadhi ya familia zikifilisika kwa sababu ya gharama ya juu ya matibabu nchini, hilo nataka liwe historia,” akasisitiza Rais Kenyatta.

Akipigia upatu serikali yake katika kujaribu kukabiliana na janga la Covid-19, Rais alitaja kiwango cha maambukizi ya virusi vya corona nchini kuwa cha chini kikilinganishwa na mataifa mengine yaliyoimarika kiuchumi.

“Ninapongeza Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe, kwa jitihada zake kujaribu kulainisha idara ya afya. Ilikuwa na uchafu mwingi sana hapo awali, amefanya kazi bora,” akasema Rais.

  • Tags

You can share this post!

Leicester City na Everton nguvu sawa ligini

Barcelona wakomoa Rayo Vallecano na kutinga robo-fainali za...