• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:46 PM
Drama Mbeyu akipokonywa ‘mic’ kwa kulaumu serikali ya Mung’aro kuchelewesha malipo ya mwanahabari aliyejitia kitanzi

Drama Mbeyu akipokonywa ‘mic’ kwa kulaumu serikali ya Mung’aro kuchelewesha malipo ya mwanahabari aliyejitia kitanzi

NA MAUREEN ONGALA

DRAMA imetokea katika mazishi ya aliyekuwa mwanahabari wa Pwani FM marehemu Sammy Ambari katika kijiji cha Mkongani, wadi ya Mastangoni baada ya Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Kilifi Gertrude Mbeyu kupokonywa maikrofoni.

Hii ni baada ya Bi Mbeyu kuanza kukosoa serikali ya Kaunti ya Kilifi kwa kuchelewesha malipo ya marehemu Ambari hali ambayo ilimfanya kupitia changamoto ya kifedha asijue la kufanya na unyonge ukamfanya kujitia kitanzi.

Mbeyu alizimwa na diwani wa wadi ya Mastangoni Hassan Mohamed ambaye alikuwa amesimama kando yake, na akampokonya maikrofoni na kumuacha Bi Mbeyu akiwa amesimama kwa mshangao.

Bi Mbeyu alimtaka diwani huyo aache kumwambia muda wake kuzungumza ulikuwa umeyoyoma.

Kulingana na Bi Mbeyu hakuna la kujutia kwani alikuwa ameambia waombolezaji kilichomsukuma mwanahabari Ambari kujitia kitanzi.

“Alidai ikashindikana, madeni yakamzidi,” akasema.

Gavana wa Kilifi pamoja na viongozi wengine akiwemo Waziri wa Jinsia Aisha Jumwa walihudhuria mazishi hayo.

Sarakasi hiyo ilisitisha ibada hiyo ya mazishi kwa zaidi ya dakika 10 huku viongozi wakijaribu kutuliza umati uliokuwa umejawa na hasira.

Kwa muda sasa Bi Mbeyu amekuwa akikosoa serikali ya kaunti kwa umma huku akimlaumu Gavana Gideon Mung’aro kwa kukosa kushughulikia matakwa ya wakazi wa Kilifi vilivyo.

Anafanya hivyo huku akiendeleza kampeni zake za kumng’atua Mung’aro katika uchaguzi mkuu wa 2027.

  • Tags

You can share this post!

Rising Starlets kukaribisha Angola uwanjani Nyayo

Rais Ruto aapa kuzima umaarufu wa ODM katika ngome ya Raila...

T L