• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 AM
Gavana Nassir awaonya wanaojihusisha na uchimbaji wa mchanga kiholela

Gavana Nassir awaonya wanaojihusisha na uchimbaji wa mchanga kiholela

NA CHARLES ONGADI

GAVANA wa Mombasa Abdulswamad Sheriff Nassir amesema atakabiliana vilivyo na matajiri wanaojihusisha na uchimbaji wa mchanga kiholela sehemu mbalimbali katika Kaunti ya Mombasa.

Akizungumza na wanahabari katika timbo la Kashani, Bamburi, katika eneoubunge la Kisauni ambako zaidi ya watu sita wanakisiwa kuaga dunia baada ya kuporomokewa na mchanga, Bw Nassir ameapa kukabiliana na matajiri hao wanaohusika katika shughuli za uchimbaji mchanga.

“Kwanza nimepiga marufuku malori kuingia katika timbo hili na ninachukua hatua hii kwa mapenzi yangu kwa wananchi,” akasema gavana.

Kwa kipindi cha wiki moja, visa vya wachimbaji kufunikwa na mchanga vimeongezeka maradufu katika matimbo mbalimbali jijini Mombasa.

Siku mbili zilizopita, afisa wa utawala eneo la Bamburi Pamela Mak’Abong’o aliwaonya wananchi dhidi ya kuendelea na shughuli za uchimbaji katika timbo hili lakini baadhi wakakaidi onyo hilo na kuendelea na shughuli zao za kawaida za uchimbaji.

Hadi tukienda mitamboni shughuli za kuwatafuta walioathiriwa na wahanga zilikuwa zikiendelea.

Tayari mwili mmoja umepatikana.

  • Tags

You can share this post!

Watu sita wafunikwa na udongo wa maporomoko ya ardhi Kisauni

Mke ajuta kutema ‘peremende’ kwa...

T L