• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
GYM za mitaani Nakuru zatajwa kama majukwaa kufunza wahalifu Karate   

GYM za mitaani Nakuru zatajwa kama majukwaa kufunza wahalifu Karate  

NA RICHARD MAOSI

MACHIFU na Wazee wa Nyumba Kumi wameombwa kuchunguza mienendo ya baadhi ya vituo vya kututumua misuli maarufu kama GYM mitaa mbalimbali Kaunti ya Nakuru, ikifichuka vinatumika kama majukwaa kufunza wahalifu Karate bila kujua.

Upekuzi wa Taifa Leo Dijitali unaonyesha maeneo yaliyopigwa darubini ni mitaa ya Kibera, Mathare Valley, Dandora, Korogocho, Mukuru kwa Njenga na Kawangware.

Nakuru, jihadhari unapozuru mitaa ya Freearea, Flamingo, Manyani, Kivumbini, Bondeni na Kaptembwo.

Imebainika kuwa wahuni wamekuwa wakijifunza namna ya kucheza miereka maarufu kama Sweep, Taekwondo, Martial Arts, Karate na Kick Boxing na hatimaye kutumia ujuzi huo kuwapiga wakazi ngeta.

Mwanandondi wa zamani Peter Njue (sio jina halisi) anasema amekuwa akifanya mazoezi katika GYM moja mtaani Bondeni, Nakuru ila haelewi mbona polisi hawajakuwa wakifanya misako huko.

Anasema baadhi yao huvalia sare za polisi, jambo linalowapa uwezo wa kufanya uhalifu wowote bila woga kama vile kukaba, kuiba na hata kuwajeruhi watu.

Washukiwa wa uhalifu wakiwa katika kituo cha Polisi cha Bondeni Nakuru wakibishana na polisi baada ya kukamatwa. PICHA|RICHARD MAOSI

Aidha, wanaweza kusoma na kupima windo lao likiwa mbali kabla ya kumparamia mtu.

Anasema mtaa wa Bondeni ni mojawapo ya maeneo ambayo visa vya uhalifu vimekithiri sana na wahusika wakitajwa kuwa vijana wadogo ambao wanajulikana.

“Hii tabia ya karibu kila kijana kushinda GYM mchana kutwa wakinyanyua vyuma na kututumua misuli inatia tumbojoto,” akasema.

Kwa upande wake, anashauri kuwa vyumba vya kufanyia mazoezi vinapaswa tu kutumika kuweka mwili katika hali nzuri kiafya, wala sio kuwahangaisha wakazi wasiokuwa na hatia

Anasema wakufunzi wa GYM za mtaani wametanguliza pesa, hivyo basi mipango kabambe inafaa kuwekwa na serikali kudhibiti vyumba vya kufanyia mazoezi.

  • Tags

You can share this post!

Shamba la kuvuna upepo Marsabit

Mwanamke Murang’a alivyoshambulia sehemu nyeti za...

T L