• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Kiwanda cha kwanza cha korosho Lamu

Kiwanda cha kwanza cha korosho Lamu

NA FARHIYA HUSSEIN

KAUNTI ya Lamu inatazamiwa kuwa na kiwanda chake cha kwanza cha korosho nchini eneo la Hindi.

Hii ni baada ya makubaliano kati ya serikali ya kaunti na mwekezaji wa kibinafsi wa Equitorial Nuts Processors.

Kulingana na Mwenyekiti wa Equitorial Nuts Bw James Wachira alionyesha imani katika mradi huo kuwa endelevu kwa vile Lamu ina korosho nyingi za kuendeleza shughuli za kiwanda.

Aidha alibainisha kuwa kiwanda hicho kitanunua karanga hizo moja kwa moja kutoka kwa wakulima, na hivyo kuwaondoa wafanyabiashara wa kati ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiwanyonya wakulima.

Katibu wa kaunti Balozi Ali Abbas alielezea uzinduzi wa mradi huo wa korosho kuwa wa thamani na ni hatua kubwa yenye matumaini kwa wakulima ambao wameshindwa kujikimu kimaisha.

Serikali ya Kaunti ya Lamu itashirikiana zaidi na mwekezaji huyo katika utekelezaji wa mpango wa kufufua korosho kwa kuanzisha mpango wa kina ambao utawawezesha wakulima kupanda miti mipya ya mikorosho kukidhi mahitaji ya kiwanda hicho.

 

  • Tags

You can share this post!

Miaka 60 ya kujitawala imepotea bure, asema Raila akitaka...

Akothee ajipongeza kwa kupata digrii licha ya kusoma kwa...

T L