• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 9:17 PM
Mwakilishi wa Nyambati akata rufaa kesi ya kuchaguliwa Nyaribo

Mwakilishi wa Nyambati akata rufaa kesi ya kuchaguliwa Nyaribo

NA WYCLIFFE NYABERI

MWANACHAMA wa United Democratic Alliance (UDA) amepeleka rufaa mahakamani kutaka kumuondoa gavana Amos Nyaribo, akidai mahakama kuu ilipuuza ushahidi aliowasilisha.

Aliyekuwa meneja wa uchaguzi (UDA) kaunti ya Nyamira Bw Dennis Omwenga Ayiera, pia alikuwa ajenti mkuu wa Bw Walter Nyambati, aliyewania ugavana Nyamira kupitia chama hicho.

Rufaa hiyo yenye kurasa 60 iliwasilishwa katika mahakama ya Rufaa mjini Kisumu, mbele ya Majaji P.O Kiage, Mumbi Ngugi na Joel Ngugi mnamo Agosti 4, 2023.

Bw Nyaribo na naibu wake Dkt James Gesami, wameorodheshwa kuwa walalamikiwa wa kwanza na pili mtawalia.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Kaunti ya Nyamira ni mlalamikiwa wa tatu na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ni mlalamikiwa wa nne.

Miongoni mwa masuala ambayo Bw Ayiera anaorodhesha katika rufaa yake ni kwamba mahakama kuu ilipuuza ushahidi aliowasilisha mahakamani kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na ufisadi na utoaji hongo kwa wapigakura.

Bw Ayiera pia alisema uchaguzi huo haukuendeshwa kwa mujibu wa sheria kama inavyohitajika kikatiba.

Mlalamishi huyo anaomba rufaa yake iruhusiwe na anaitaka mahakama ibatilishe uchaguzi wa Bw Nyaribo.

Na Dkt Gesami kawa gavana na naibu gavana na uchaguzi mpya ufanyike.

“Malalamiko mbele ya mahakama ya rufaa yaruhusiwe na uchaguzi wa mlalamikiwa wa kwanza na wa pili kama gavana na naibu wa gavana ubatilishwe. Uchaguzi mpya wa ugavana ufanyike Nyamira ndani ya siku 60 kuanzia tarehe ya uamuzi,” ilisema sehemu ya Ombi la Bw Ayiera.

Gavana Nyaribo na naibu wake walipotangazwa washindi wa kinyang’anyiro cha ugavana, Bw Ayiera alipinga uamuzi huo katika Mahakama ya Juu lakini ombi lake likatupiliwa mbali na Jaji Kanyi Kimondo kwa msingi kwamba hakuwa na ushahidi wa kutosha.

Wakati alitoa uamuzi wake Februari mwaka huu, Jaji Kimondo pia alibainisha kuwa mleta maombi hakuthibitisha pasipo shaka kuwa mlalamikiwa wa kwanza na wa pili walitumia rasilimali za umma kuwashawishi wapiga kura wawapigie kura.

Katika uchaguzi wa mwaka jana, Bw Nyaribo (United Progressive Alliance) alipata kura 82,090 dhidi ya Bw Nyambati aliyepata kura 49, 281.

 

  • Tags

You can share this post!

AMINI USIAMINI: Kakakuona humeza mawe iwe rahisi chakula...

Shakahola: Waliookolewa wageuzwa kuwa mashahidi

T L