• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 1:02 PM
Serikali kutumia Sh7 bilioni kuhamisha makaburi na madhabahu kujenga bwawa

Serikali kutumia Sh7 bilioni kuhamisha makaburi na madhabahu kujenga bwawa

Na SIAGO CECE

SERIKALI imepanga kutumia Sh7 milioni kuhamisha makaburi na madhabahu ya kitamaduni katika Kaunti ya Kwale, ili kupisha ujenzi wa Bwawa la Mwache ambao umeratibiwa kuanza Februari.

Baadhi ya wenyeji walikuwa wamelalamika kuwa uharibifu wa sehemu hizo utasababisha majanga tele zaidi katika siku za usoni.

“Mchakato huu ni wa gharama kubwa. Tunatumia kiwango kikubwa cha fedha kuhamisha makaburi na kaya ambazo ni nyingi. Pia tuna miti ya kihistoria ambayo inahamishwa,” Bw Irungu alisema.

Ujenzi wa bwawa hilo utakaogharimu takriban Sh20 bilioni unafanywa katika eneobunge la Kinango, Kaunti ya Kwale.Ulikuwa umecheleweshwa kwa miaka sita kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ulipaji fidia kwa wamiliki wa ardhi.

‘Takriban asilimia 75 ya wakazi wamefidiwa ili kuhakikisha kwamba mradi huo unaanza,” akasema Bw Irungu.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Bw Irungu alisema wakazi 12,000 wanatarajiwa kuhamishwa ili kutoa nafasi ya mradi huo.

You can share this post!

NJENJE: Pakistan yaibuka mtumizi bora wa chai ya Kenya,...

Kigame kuzindua muungano

T L