• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:47 PM
Wakulima wa kahawa kusubiri zaidi viwanda vikarabatiwe

Wakulima wa kahawa kusubiri zaidi viwanda vikarabatiwe

Na GITONGA MARETE

WAKULIMA wa kahawa katika Kaunti ya Meru watalazimika kusubiri kwa muda zaidi viwanda vya kahawa vilivyoko katika hali mbaya vikarabatiwe, baada ya kandarasi za kampuni zilizokuwa zikiendeleza ujenzi huo kufutiliwa mbali.

Zaidi ya viwanda 50 katika kaunti hiyo vilifaa vikarabatiwe kwa kati ya Sh10 milioni hadi Sh32 milioni kwa kila kiwanda kulingana na kiwango cha kazi.

Hata hivyo, kandarasi hizo zilifutiliwa mbali kutokana na kazi duni na pia kampuni hizo kudai zilipwe asilimia 35 za fedha kwanza kabla ya kuendelea na kazi.

“Tumekamilisha baadhi ya viwanda katika kaunti ya Tharaka Nithi ila tatizo ni katika Kaunti ya Meru ambapo baadhi ya wanakandarasi walipata kazi zao kupitia mawakala. Wamefanya miradi hiyo ijikokote mno,” akasema Mratibu wa miradi hiyo Caroline Karanja.

Ukarabati wa viwanda hivyo unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Mauzo ya Kahawa ( ICO) kwa kushirikiana na wakulima ambao wanahusika na kilimo cha mimea hiyo. Hata hivyo, meneja wa vyama vya ushirika vya ushirika vya kahawa walisema mradi huo ulizingirwa na utata na hawakuhusishwa katika kuwateua wanakandarasi hao.

Bi Karanja naye alitofautiana na mameneja hao, akisema kuwa waliamua kuwasaka wanakandarasi hao ili kuzuia ufisadi ambao ungetokea. Wizara ya Kilimo ya Kaunti ya Meru pia ilisema kuwa haikushirikishwa katika mchakato wa ukarabati huo.

You can share this post!

Barabara ya Broadway Thika yakaribia kukamilika

Niko tayari kumenyana na mradi wa Uhuru, Ruto asema

T L