• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 6:43 AM
Wanaharakati washinikiza mkuu wa TSC Nancy Macharia ajiuzulu

Wanaharakati washinikiza mkuu wa TSC Nancy Macharia ajiuzulu

NA WINNIE ONYANDO

KIKUNDI cha Bunge la Mwananchi sasa kinamtaka Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC), Nancy Macharia ajiuzulu.

Kikundi hicho kikiongozwa na Francis Awino kinadai kuwa Bi Macharia anadhalilisha juhudi za Rais William Ruto za kudhibiti ufisadi nchini.

Kulingana na kundi hilo, ufisadi unatawala tume hiyo inayoongozwa na Bi Macharia.

“Tunamtaka Bi Macharia ajiuzulu kwa kuwa ameshindwa kukabiliana na ufisadi katika tume hiyo,” akasema Bw Awino.

Bw Awino tayari amewasilisha malalamishi yao katika Mahakama Kuu.

Kulingana na karatasi za korti, Bw Awino alidai afisi ya mkuu huyo wa TSC imekumbwa na madai ya ukiukaji wa sheria.

“Kama kikundi cha wanabunge, tunataka mkuu huyo ajiuzulu kwani tume hiyo inakumbwa na ufisadi. Ikiwa hatafanya hivyo, basi tutaandamana,” akasema Bw Awino.

Kadhalika, Awino alisema katika ombi lake kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alihusisha TSC katika kashfa ya mishahara ya Sh3 bilioni ambapo Mkurugenzi Mtendaji huyo alilipa wafanyikazi licha ya kwamba shirika hilo lilikuwa na uhaba wa walimu.

Aidha, Awino alisema ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inabainisha kuwa mapitio ya uchambuzi wa kina wa orodha ya mishahara kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 ulibaini kuwa walimu 32 hawakuwa wamepokea mshahara wa jumla ya Sh33,780,614.

  • Tags

You can share this post!

Wazee Lamu wataka serikali kuwachunguza wanasiasa wenye...

AMINI USIAMINI: Thorny devil ni mjusi ambaye hunywa maji...

T L