• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 7:53 PM
DJ Fatxo: DCI walikubali hatukumfanyia ushoga wala kumtoa kafara Jeff Mwathi

DJ Fatxo: DCI walikubali hatukumfanyia ushoga wala kumtoa kafara Jeff Mwathi

NA MWANGI MUIRURI

MCHEZA santuri Lawrence Njuguna Wagura ‘DJ Fatxo’ amejitokeza tena kufichua kwamba uchunguzi wa kimaabara katika makalio ya Jeff Mwathi ulifichua kwamba hakuwa ametekelezewa ushoga.

Aidha, DJ Fatxo alikana madai kwamba alimtoa Bw Mwathi kafara.

Kijana Mwathi alipatikana ameaga dunia katika makazi ya msanii huyo.

Haikueleweka mara moja ikiwa, Mwathi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 23 aliruka kutoka ghorofa ya saba, akajitoa uhai, ama alirushwa kimakusudi akiwa hai au maiti.

DJ Fatxo alifichua kwamba Mwathi alionekana katika kamera za siri akitoka kwa dirisha akiwa ameshika simu yake mkononi kwa njia iliyoonekana kuwa ya hiari.

Katika uchunguzi uliozinduliwa na maafisa wa uchunguzi wa jinai (DCI) DJ Fatxo, dereva wake na pia binamuye, wote wakiwa wanaume waliorodheshwa kama washukiwa.

“Sasa imedhihirika wazi hatukuhusika. Ripoti za uchunguzi za DCI zilituondolea lawama. Haswa Mimi: Sikuhusika kamwe licha ya kudhaniwa katika mitandao na kusulubiwa kama muuaji,” akasema katika mahojiano na msanii Eric Obinna.

Kuhusu ni kwa nini mwili wa Mwathi ulipatikana ukiwa uchi kuanzia kiunoni kwenda chini, DJ Fatxo alifichua kwamba DCI walitafsiri kwamba long’i yake aidha ilitoka akijipenyeza alikorukia au ikatolewa na upepo.

“Katika hali ya kuruka, DCI walitafsiri kwamba nguo zake zilimhudumia kama parachuti na nguvu za upepo huenda zilimtoa long’i,” akasema.

Alisema kwamba uchunguzi wa DCI pia ulimtenganisha na washukiwa hao wengine wawili, baada ya simu zao kutwaliwa na pia kuzimwa kutangamana ili wasihujumu uchunguzi.

DJ Fatxo alisema kwamba anatamani sana kurejelea utulivu na umaarufu wake wa usanii.

  • Tags

You can share this post!

Nairobi City Marathon 2023  

Serikali kuondoa masoko yaliyoko kandokando mwa barabara...

T L