• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Karua atangaza mipango ya maandamano leo Alhamisi

Karua atangaza mipango ya maandamano leo Alhamisi

NA CHARLES WASONGA

MUUNGANO wa Azimio la Umoja-One Kenya umewaagiza wafuasi wake kujiandaa kwa siku ya pili ya awamu ya tatu ya maandamano dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza leo Alhamisi, Julai 20,2023.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, kinara mwenza wa muungano huo Martha Karua mnamo Jumatano aliwapongeza wafuasi wao waliojitokeza kushiriki maandamano ya Jumatano, Julai 19, 2023 katika maeneo mbalimbali nchini.

“Tungependa kuwaomba wakombozi jioni ya leo (Jumatano) kwamba ni wakati sasa wa kurejea nyumba, kuongeza nguvu tayari kwa maandamano kesho (leo Alhamisi Julai 20, 2023), siku ya pili ya wimbi la tatu la maandamano,” akasema.

Hata hivyo, Bi Karua ambaye pia ndiye kiongozi wa Narc Kenya, alisikitika kuwa polisi waliwajeruhi na hata kuwaua baadhi ya waandamanaji ambao hawakuwa na silaha zozote.

“Tunasema pole kwa wenzetu ambao wamewapoteza wapendwa wao waliopigwa risasi na polisi katili. Aidha, tunawatakia afueni ya haraka wale ambao walijeruhiwa na wamelazwa katika hospitali mbali mbali wakipokea matibabu,” akasema .

Hata hivyo, Bi Karua alitoa wito kwa Wakenya kujitokeza kwa wingi kufanya maandamano ya amani katika maeneo wanakoishi.

“Jijini Nairobi watu watakusanyika katika uwanja wa Huruma, uwanja wa Kangemi na katika uwanja wa Central Park, katikati mwa jiji. Tunaraji kwamba maafisa wa polisi watatoa usalama kwa waandamanaji,” akasema.

Alisema wale ambao hawatapata muda Alhamisi wanaweza kushiriki maandamano hata siku ya Ijumaa, Julai 21, 2023.

“Aluta Continua (Mapambano yanaendelea),” Bi Karua akasema.

  • Tags

You can share this post!

Mwanaharakati ashtakiwa kwa kula njama kumtimua Rais...

Omanyala atua mjini Monaco kuwinda ushindi katika Diamond...

T L