• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Omanyala atua mjini Monaco kuwinda ushindi katika Diamond League

Omanyala atua mjini Monaco kuwinda ushindi katika Diamond League

NA GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Afrika na Jumuiya ya Madola mbio za mita 100, Ferdinand Omanyala amewasili jijini Monaco tayari kwa riadha za Diamond League zitakazofanyika mnamo Julai 21.

Afisa huyo wa polisi alikamilisha mazoezi ya humu nchini Jumanne ugani Kasarani kabla ya kuelekea Monaco kwa duru hiyo ya tisa.

“Nimefika salama hapa Monaco tayari. Nitakutana wakimbiaji watajika kwenye Monaco Diamond League ambako natarajia kufyatuka kasi ya juu sana Ijumaa,” alieleza Taifa Spoti mnamo Jumatano.

Omanyala atafufua uhasama na raia wa Afrika Kusini Akani Simbine na bingwa wa dunia mbio za chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20, Letsile Tebogo kutoka Botswana, miongoni mwa wengine.

Simbine alishikilia rekodi ya Afrika na mataji ya Afrika na Jumuiya ya Madola kabla ya Omanyala kumpokonya akimaliza Kip Keino Classic Continental Tour katika nafasi ya pili mwaka 2021 na kuibuka bingwa wa Afrika na Jumuiya ya Madola mwaka 2022.

“Nitakuwa mjini Miramas, Ufaransa pekee yangu, ingawa natumai kuwa Shirikisho la Riadha Kenya litaleta washiriki wengine wa mbio fupi hapa mapema kufanyia mazoezi yao hapa,” alisema Omanyala ambaye atashiriki mashindano mawili kabla ya kuzamia matayarisho ya Riadha za Dunia zitakazofanyika Agosti 19-27 jijini Budapest, Hungary.

Anasema kuwa klabu ya riadha ya Miramas itagharimia sehemu ya maandalizi yake mjini humo.

Omanyala ameshiriki duru za Diamond League za Rabat (Morocco), Florence (Italia) na Paris (Ufaransa), ingawa bado hajaonja ushindi. Alikamata nafasi ya tatu Rabat na ya pili Florence na Paris.

  • Tags

You can share this post!

Karua atangaza mipango ya maandamano leo Alhamisi

Seneti yashangazwa na idadi kubwa ya makaimu serikalini

T L