• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Katibu aliyeshtakiwa kumpiga mke mbele ya watoto ana kesi ya kujibu

Katibu aliyeshtakiwa kumpiga mke mbele ya watoto ana kesi ya kujibu

NA RICHARD MUNGUTI

KATIBU wa masuala ya Baraza la Mawaziri Julius Korir anayeshtakiwa kumchapa na kumuumiza mkewe waliyetengana yuko na kesi ya kujibu.

Hakimu mkazi mahakama ya Milimani Dolphin Alego alisema upande wa mashtaka umewasilisha ushahidi wa kutosha kuwezesha mahakama kumwagiza Bw Korir ajitetee.

Bw Korir amekana shtaka la kumchapa na kumjeruhi Evelyn Koech.

Bi Alego alimwagiza Bw Korir ajitetee Agosti 25, 2023 kabla ya hukumu kupitishwa.

“Baada ya kutathmini ushahidi wote uliowasilishwa na upande wa mashtaka, hii mahakama imekupata na kesi ya kujibu. Utajitetea Agosti 25,2023,” Bi Alego alisema katika uamuzi wake.

Bw Korir ambaye yuko nje kwa dhamana, anakabiliwa na shtaka la kumpiga na kumjeruhi Evelyne Koech mnamo Septemba 17, 2020, katika mtaa wa kifahari wa Karen.

Alipotoa ushahidi, Evelyne aliambia mahakama alikuwa mjamzito alipotandikwa na kuumizwa mbele ya watoto.

  • Tags

You can share this post!

Hakuna maandamano kesho Jumatano – IG Koome

Wakazi watilia shaka usalama wao kambini Juhudi Primary

T L