• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Kindiki: Polisi kusalia Kaskazini mwa Bonde la Ufa hata baada ya oparesheni

Kindiki: Polisi kusalia Kaskazini mwa Bonde la Ufa hata baada ya oparesheni

Na WANGU KANURI

POLISI waliotumwa katika eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa mnamo Februari watasalia mumo humo.

Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Prof Kithure Kindiki alipokuwa akielezea seneti alisema kuwa maafisa hao wamekita kambi katika kaunti za Samburu, Turkana, Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet.

Kaunti hizo ndizo wezi wa mifugo hujifichia. “Hali ya usalama Samburu imeimarika baada ya wanajeshi kutumwa huko kuwasaidia maafisa wa polisi. Tumeweza kugundua maeneo kadha wa kadha katika kaunti hiyo pamoja na kaunti zingine ambazo wezi hawa wa mifugo wanajificha,” Prof Kindiki akaelezea wabunge.

Aliongezea, “Maafisa hao watasalia mumo humo hata baada ya kusitisha oparesheni hiyo. Watabaki katika maeneo hayo ili iwe ngumu kwa wezi hao wa mifugo kushambulia watu tena.”

Isitoshe, Prof Kindiki aliripoti kuwa oparesheni hiyo imekuwa nzuri huku akiwahakikishia kuwa wezi hao wa mifugo hawatajificha kwenye mapango waliyokuwa wakitumia ili kupanga mashambulizi.

Mnamo Machi, serikali ilitangaza wizi wa mifugo kama janga nchini na kuwalazimisha wakazi wa maeneo hayo yaliyogomea na wezi hao kuondoka kule.

Hii ni baada ya Rais William Ruto kuamrisha Wanajeshi wa Kenya (KDF) na Huduma ya Polisi (NPS) kushirikiana katika oparesheni ya usalama katika kaunti hizo zilizoathirika na wizi wa mifugo.

 

  • Tags

You can share this post!

Mashindano ya vijana ya KYISA yapamba moto Tharaka-Nithi

Eric Omondi anyakwa na polisi Kisumu kwa kuandaa maandamano

T L