• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Eric Omondi anyakwa na polisi Kisumu kwa kuandaa maandamano

Eric Omondi anyakwa na polisi Kisumu kwa kuandaa maandamano

MWANDISHI WETU

MCHESHI Eric Omondi ametiwa mbaroni katika kaunti ya Kisumu baada ya kuongoza maandamano ya amani eneo hilo.

Bw Omondi alikuwa akiongoza wanafunzi wa vyuo vikuu katika maandamano hayo yaliyokuwa yamelenga kulalamikia gharama ya juu ya maisha, ongezeko la karo ya shule na ukosaji wa ajira kwa Wakenya.

Kulingana na video iliyonaswa na Plug TV, mchekeshaji huyo pamoja na waandamanaji wenzake walionekana wakifunga barabara wakiimba nyimbo za maandamano.

Isitoshe, Bw Omondi aliwashauri wengine wao kutandaza godoro kwa barabara na kulala chini.

Wiki mbili zilizopita katika kaunti ya Nairobi, Bw Omondi aliongoza maamndamano lakini maafisa wa fanya fujo uone wakamzingira kabla ya kurusha vitoa machozi ili kutawanya waandamanaji hao.

Baadaye, Bw Omondi alikamatwa na kufikishwa kortini kwa kosa la kusababisha vurugu kwa kuweka kizuizi katika barabara ya Kenyatta Avenue, Nairobi na kuwazuia watu wengine matumizi ya barabara.

Hata hivyo, alikana mbele ya hakimu mwandamizi Bi Zainabu Abdul kwamba alisababisha vurugu kwa kupiga kelele kuhusu bei ya unga.

“Mheshimiwa nimeshtakiwa kwa nini ilhali Kipengele 37 cha Katiba kinaruhusu maandamano na kupiga kelele ikiwa haki imekandamizwa,” Omondi alishangaa kortini

Pia alieleza masikitiko kwamba ameshtakiwa ilhali muungano wa Azimio na serikali ya Kenya Kwanza umekubaliana kusitisha maandamano na hata wanasiasa walioshtakiwa Kiambu waliachiliwa.

  • Tags

You can share this post!

Kindiki: Polisi kusalia Kaskazini mwa Bonde la Ufa hata...

Mkurugenzi wa kampuni ashtakiwa kupora shamba la Jimi...

T L