• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:02 PM
Magoha ashangaza kufunga shule ghafla

Magoha ashangaza kufunga shule ghafla

NA WANDERI KAMAU

WAZAZI na walimu nchini Jumatatu walijipata kwenye njiapanda, baada ya Waziri wa Elimu George Magoha kutangaza kuwa wanafunzi wataenda kwenye mapumziko ya muhula wa pili kuanzia leo Jumanne hadi Alhamisi wiki ijayo.

“Wazazi wanaagizwa kuhakikisha kuwa wanao wameenda majumbani kwa mapumziko ya muhula kuanzia Jumanne, Agosti 2 hadi Alhamisi 11, Agosti 2022,” akasema Prof Magoha kwenye taarifa.

Hii inamaanisha shule zitafunguliwa siku moja tu baada ya upigaji kura, jambo ambalo wazazi walilalamikia vikali jana.

“Magoha amesahau kuja Covid-19 na madarasa yanapasa kupuliziwa dawa kabla wanafunzi warudi? Pia anasahau huenda kukawa na taharuki ambayo inaweza kutatiza usafiri,” akalalamika mzazi Munguti Richard jijini Nairobi.

“Hili ni agizo ambalo limetupata tukiwa hatujajitayarisha. Ni hali itakayotulazimu kupangua mipango yetu, hasa kifedha,” akasema Bi Vivian Kerubo, ambaye ni mkazi wa eneo la Mwiki, Kaunti ya Kiambu.

Kwenye taarifa Jumatatu, waziri alisema hatua hiyo ni kuhakikisha kuwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu hapo Jumanne ijayo yataendeshwa bila matatizo yoyote.

Shule za umma ni baadhi ya maeneo yatakayotumika kama vituo vya kupigia na kuhesabia kura.

  • Tags

You can share this post!

Kenya Kwanza wammezea mate Shahbal

Miungano yatishia usalama kwa uvumi

T L