• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Makali Mulu ndiye mkali wao kwa kushiriki mijadala Bungeni

Makali Mulu ndiye mkali wao kwa kushiriki mijadala Bungeni

NA CHARLES WASONGA

MBUNGE wa Kitui ya Kati Dkt Makali Mulu ameibuka kuwa mchapa kazi zaidi katika Bunge la 13 tangu bunge hilo kuanza vikao vyake Septemba 17, 2022.

Hii ni kulingana na ripoti iliyotolewa Jumatano na shirika linalofuatilia utendakazi wa Bunge, Mzalendo Trust. Wabunge wengine ambayo wameng’aa bungeni kufikia sasa ni; Beatrice Elachi (Dagoretti Kaskazini), James Nyikali (Seme) na Ken Chonga (Kilifi Kusini).

Kulingana na ripoti hiyo iliyotiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Caroline Gaita, wabunge hawa walichangia kwa wingi mijadala kuhusu masuala yenye umuhimu wa kitaifa.

Masuala hayo ni kama vile kupanda kwa gharama ya maisha, ukosefu wa ajira kwa vijana, ukame, masuala ya bajeti miongoni mwa masuala mengine.

“Wakenya walipiga kura mnamo Agosti 9, 2023 wakiwa na matarajio makubwa kwamba wabunge wao wangeangazia changamoto zinazowahusu. Ni masuala kama ya ukosefu wa ajira, kupanda kwa gharama ya maisha miongoni mwa masuala mengine. Uchanganuzi wa Mzalendo Trust umebaini kuwa wabunge Makali Mulu, Beatrice Elachi, James Nyikal na Ken Chonga walitia fora,” akasema Bi Gaita.

Katika bunge la Seneti, Seneta wa Nandi Samson Cherargei ameorodheshwa kama mchangiaji bora zaidi akifuatwa na Eddy Oketch (Migori), John Kinyua (Laikipia) na seneta Mohamed Faki (Mombasa) kwa usanjari huo.

“Baadhi ya masuala ambayo maseneta walijadili ni dhuluma za kihistoria, afya ya kiakili na elimu ya watoto wanaoishi na aina mbalimbali za ulemavu,” inasema ripoti hiyo ya Mzalendo Trust.

  • Tags

You can share this post!

Namwamba awatuza wanahabari kwenye hafla ya kufana

Siku tano za wali na nyama

T L