• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Raia 2 wa kigeni washtakiwa kwa kupatikana na bhangi na dhahabu feki  

Raia 2 wa kigeni washtakiwa kwa kupatikana na bhangi na dhahabu feki  

 

Na RICHARD MUNGUTI

RAIA wawili wa Congo waliokutwa wakichangamkia misokoto 13 ya bhangi wameshtakiwa kwa kushiriki biashara feki ya dhahabu na pia kupatikana na mihadarati.

Mathew Bayindu Patsum na Mercelin Wa Nyanguangu Bruce, walishtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Lucas Onyina.

Mathew na Mercelin walikabiliwa na mashtaka ya kulaghai kampuni iliyoko mjini Seol, nchini Korea USD 214, 500 sawa na Sh27, 585, 000 thamani ya Kenya, wakidai wangeliitumia kilo 175 za dhahabu.

Wawili hao walieleza kampuni hiyo wataipelekea dhahabu hiyo kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Kampuni ya Tophead Vision Company Limited (TVCL) iliyo na afisi zake kuu Seol, Korea ilikuwa imeelezwa kuwa itapelekewa dhahabu hiyo kutoka JKIA punde tu itakapowasili kutoka nchi ya DRC.

Mawakili Ishmael Nyaribo na Victor Mosota waliomba Mathew na Mercelin waliomba washtakiwa waachiliwe kwa dhamana.

Kiongozi wa mashtaka, Anderson Gikunda alipinga ombi hilo la dhamana akisema “hawana makazi yanayojulikana hapa Kenya.”

Hakimu Onyina atatoa uamuzi wa ombi hilo la dhamana Aprili 14, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Aomba aachiliwe huru kuendeleza biashara ya dhahabu feki

Waandishi habari hawatashikilia vyeo MCK, asema waziri

T L