• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 3:55 PM
Aomba aachiliwe huru kuendeleza biashara ya dhahabu feki

Aomba aachiliwe huru kuendeleza biashara ya dhahabu feki

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA imeombwa imwachilie huru raia wa Liberia anayeshtakiwa kwa kumtapeli mfanyabiashara wa kimataifa USD 408, 229 sawa na Sh57 milioni thamani ya Kenya, akidai atampelekea dhahabu kilo 6.483 nchini Korea.

Joseph Bedell mwenye umri wa miaka 57 aliomba korti imwachilie kupitia kwa mawakili Ishmael Nyaribo na Victor Mosota kwa vile haina mamlaka ya kusikiliza kesi inayomkabili.

Nyaribo na Mosota walimweleza hakimu mkuu mahakama ya Milimani Lucas Onyina kwa Bedell hajulikani alifanya uhalifu huo nchi ipi ulimwenguni.

“Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma Noordin Haji hajasema katika cheti cha mashtaka uhalifu ulifanyika nchi gani,” Nyaribo aliambia mahakama.

Wakili huyo alisema makosa ya mshtakiwa ni kupatikana katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Bedell anadaiwa alimweleza mteja wake Bw Shanmugam Sundar Darmaraju dhahabu aliyokuwa amtumie imeshikwa na maafisa wa forodha katika uwanja wa JKIA mnamo Aprili 4, 2023.

Lakini kiongozi wa mashtaka alipinga ombi hilo akisema, mshtakiwa alipatikana nchini kinyume cha sheria na alikuwa anashiriki katika biashara feki ya dhahabu.

Mshtakiwa alizuiliwa hadi Aprili 17, 2023, korti iamue ikiwa itamwachilia au la.

  • Tags

You can share this post!

Maandamano yaendelee sambamba na mazungumzo – Raila

Raia 2 wa kigeni washtakiwa kwa kupatikana na bhangi na...

T L