• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Sabina Chege ajutia kuwa kibaraka wa Kenyatta 2022, asema angemsikiza Ruto angekuwa naibu gavana Nairobi

Sabina Chege ajutia kuwa kibaraka wa Kenyatta 2022, asema angemsikiza Ruto angekuwa naibu gavana Nairobi

NA MWANGI MUIRURI

MBUNGE maalum Bi Sabina Chege amefichua kwamba William Ruto alikuwa amemuahidi asilimia 40 ya mamlaka ya Nairobi angekubali kuwa mgombea mwenza wa Johnson Sakaja katika uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

Bi Chege alifichua kwamba Bw Ruto wakati huo alikuwa akisaka washirika wa kumsaidia kushinda urais na hatimaye kuwa na udhibiti wa jiji kuu.

“Nilikuwa niwe Naibu Gavana wa Nairobi na hatimaye niwe kinara wa asilimia 40 ya serikali ya Sakaja. Nilikataa kwa kuwa imani yangu ya kisiasa ilikuwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na mgombezi wetu wa urais Raila Odinga,” akasema.

Bi Chege aidha alikuwa ametoa ishara za kuwania ugavana Murang’a, akabadili nia na ikaonekana kana kwamba alilenga ubunge wa Kigumo au atetee wadhifa wake wa mbunge wa kaunti kwa awamu ya tatu.

Mwishowe alisema kwamba alikuwa ametupilia mbali hoja hizo zote na kuamua kuchapa siasa za Azimio la Umoja – One Kenya akilenga kuhudumu katika safu ya kitaifa.

“Hata hivyo, mambo yalitwendea mrama tuliposhindwa na Rais Ruto na hivyo ndivyo nilipoteza nafasi hizo zilizokuwa wazi kwangu.

“Nilikubali kwa kuwa asiyekubali kushindwa sio mshindani na leo hii mimi nimeamua kushirikiana na serikali,” akasema mbunge huyo maalum.

Nafasi yake Nairobi ilitwaliwa na Bw James Muchiri kutoka Kaunti ya Nyandarua na wakashinda uchaguzi huo ndani ya chama cha United Democratic Alliance (UDA), Gavana akiwa ni Bw Sakaja.

 

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Yaya mshukiwa wa wizi wa watoto Nakuru akamatwa Nairobi

Ofisi za Omtatah zavunjwa usiku

T L