• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 6:24 PM
Yaya mshukiwa wa wizi wa watoto Nakuru akamatwa Nairobi

Yaya mshukiwa wa wizi wa watoto Nakuru akamatwa Nairobi

NA MERCY KOSKEI

MAAFISA wa upelelezi mjini Nakuru wanamzuilia mfanyakazi mwenye umri wa miaka 20 anayeshukiwa kuiba mtoto wa mwajiri wake mnamo Jumatano Julai, 19 kabla ya kutorokea Nairobi.

Mshukiwa huyo aliyetambuliwa kama Brenda Apalat, alikamatwa na maafisa DCI mnamo Ijumaa Julai 21, 2023 akiwa ameabiri matatu eneo la Ngata akielekea Busia.

Kulingana na mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai Kaunti Ndogo ya Nakuru Mashariki, George Momanyi, walipokea habari kutoka kwa mamake mtoto Bi Lena Nyambura kwamba yaya huyo alikuwa ametoroka na mtoto wake wa miaka miwili na nusu.

Alisema kuwa walianza uchunguzi wao na mawimbi ya simu ya mshukiwa yalionyesha alikuwa Nairobi.

Siku ya Alhamisi asubuhi simu yake ilionekana akiwa katika kituo cha basi jijini.

Bw Momanyi alisema kuwa waliendelea kufuatilia mshukiwa huyo hadi alipofika Nakuru, matatu kadhaa zilisimamishwa ili kumsaka.

Bw Momanyi alisema kuwa maafisa wa upelelezi walipopekua matatu aina ya Nissan, mshukiwa na mtoto walipatikana na wote wawili walitambuliwa na Bi Nyambura.

“Tulipopata taarifa kutoka kwa Nyambura, mkazi wa eneo la Free Area, timu yetu ilisonga kwa kasi.

“Tumekuwa tukimfuatilia kwa karibu hadi alipofika Nakuru na kukamatwa,” akasema Bw Momanyi.

Alifichua kuwa Bi Nyambura alifahamisha polisi kwamba alimwacha mtoto wake chini ya ulinzi wa yaya huyo ambaye alikuwa amefanyia kazi kwa siku nne pekee.

Bi Nyambura alieleza polisi kwamba alishtuka aliporudi jioni na kupata wawili hao wametoweka.

Alielekea katika kituo cha polisi Free Area kuripoti.

“Tumeanzisha Uchunguzi kubaini sababu ya kufanya hivyo. Tunataka kujua ikiwa ni kundi linalohusishwa na wizi wa watoto,” alisema

Mshukiwa atafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu na kushtakiwa kwa kosa la kuiba mtoto kinyume na kifungu cha 174(1)(a) cha kanuni ya sheria.

 

  • Tags

You can share this post!

Ruto awataka viongozi wa Azimio kutuma watoto wao kuongoza...

Sabina Chege ajutia kuwa kibaraka wa Kenyatta 2022, asema...

T L