• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Serikali kuajiri walimu 20,000

Serikali kuajiri walimu 20,000

NA WINNIE ATIENO

SERIKALI imeeleza kuwa itawaajiri takriban walimu 20,000 waliohitimu ili kupunguza uhaba wa walimu kote nchini.

Akizungumza katika kongamano la walimu wakuu wa shule za upili katika shule ya Upili ya Sheikh Khalifa bin Zayed jijini Mombasa, Mwenyekiti wa Tume ya kuwaajiri Walimu (TSC), Bw Jamleck Muturi alisema tume hiyo itawaajiri walimu wa sekondari na hata wa shule za msingi kuziba pengo hilo.

Kulingana naye serikali imetenga Sh4.6 bilioni kuajiri walimu, Sh1 bilioni kuwapandisha ngazi walimu na Sh1.3 bilioni kuwapa mafunzo ya mtaala mpya wa utendaji na umilisi.

“TSC ilipata kiasi kizuri cha pesa katika mgao wa bajeti. Tulipata Sh323.7 bilioni ambazo ni ongezeko la Sh24 bilioni za mwaka uliopita. Sh4.6bn zitatumika kuwaajiri walimu wa kandarasi. Tangazo litatolewa kufikia wiki ijayo.”

  • Tags

You can share this post!

Kiptoo aingia Nairobi City Marathon washiriki wakigonga...

Patrick ‘Jungle’ Wainaina amchanua Ruto namna ya...

T L