• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
Serikali yabuni njia ya kujua vitabu feki, vitabu vipya vya Fasihi vyatoka

Serikali yabuni njia ya kujua vitabu feki, vitabu vipya vya Fasihi vyatoka

Na FAITH NYAMAI

WAZAZI sasa watakuwa na uwezo wa kubaini vitabu feki wanapoelekea madukani kuwanunulia watoto wao vitabu vipya vinavyohitajika kwa masomo mbalimbali shuleni.

Hii ni kupitia kutuma nambari iliyoko kwenye kitabu walichonunua kwa nambari 22776 kwa simu ya mkononi.

Lengo la huduma hiyo ambayo imekumbatiwa na wizara ya elimu ni kuhakikisha kuwa shule, wazazi na hata wanafunzi wenyewe wanatumia vitabu ambavyo vimeidhinishwa pekee.

“Tunalenga kuhakikisha kuwa vitabu vilivyoidhinishwa kutumika kwenye silabasi pekee ndivyo vinavyonunuliwa,” akasema Katibu katika wizara hiyo Dkt Julius Jwan.

Wakati huo huo, wizara hiyo ilitangaza rasmi vitabu vipya vya kiada ambavyo vitatahiniwa kwa wanafunzi wa kidato cha nne kwa muda wa miaka mitano ijayo. Vitabu hivyo ni vya fasihi ya Kiswahili na Kingereza.

Katika Kiswahili, vitabu ambavyo vitatahiniwa ni Bembea (Riwaya) cha Dkt Timothy Moriasi, Mapambazuko na Hadithi Nyingine (Hadithi Fupi) na Nguu za Jadi (Tamthilia). Vimechukua sehemu ya Kigigo (Riwaya,) Tumbo Lilisiloshiba na Hadithi Nyingine (Hadithi Fupi) na Chozi la Heri (Tamthilia).

Katika fasihi ya Kingereza vitabu vitakavyotahiniwa kwa lazima ni Fathers of Nations na The Samaritan. Vile mtahiniwa atachagua kufanya kwa hiari yake ni Floating World, A silent Song and Other Stories ( hadithi fupi) na A Parliament of Owls.

Vitabu hivyo vitatahiniwa kati ya 2022 na 2026.

You can share this post!

GUMZO: PSG sasa yaipiku Madrid katika mbio za kumtwaa Pogba

Tutasaidia IEBC kuendesha uchaguzi huru na haki –...

T L