• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Serikali yaonya wakuu shuleni dhidi ya kuongeza karo

Serikali yaonya wakuu shuleni dhidi ya kuongeza karo

NA WINNIE ATIENO

SERIKALI imepiga marufuku wakuu wa shule kuongeza karo ya shule za msingi na za sekondari msingi (JSS).

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alieleza kuwa karo ya shule za mabweni pia itasalia ilivyo kwa sasa.

Akizungumza Jumatano wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la walimu wakuu wa shule za msingi katika shule ya msingi ya Sheikh Khalifa Bin Zayed jijini Mombasa, Bw Machogu alieleza kuwa serikali haitaongeza karo kwa shule zote kwa sasa.

“Serikali ya Rais William Ruto haina lengo la kuongeza karo ya shule za Sekondari msingi na zile za upili . Karo ya shule za mabweni zitasalia kama ilivyopitishwa,” akasema Bw Machogu.

Bw Machogu alinukuu kipenge cha 53 cha katiba kinachosema elimu ya msingi ni ya bure na ya lazima.

“Yeyote anayefanya hilo atakuwa ameenda kinyume na Katiba yetu. Yeyote ambaye hataki kuwa mkuu wa shule, hatukulazimishi, waweza kujiuzulu. Kuna Wakenya wengi ambao wanataka kupata nafasi hizo na wana uwezo wa kufuata sheria,” akasema.

Waziri huyo, alisema wakuu wa shule walikuwa wamekiuka sheria kwa kutoza karo ya Sh200,000 kila mwaka huku wengine wakitoza Sh150,000.

“Elimu ilikuwa imekuwa ghali sana kwa Wakenya wengi. Ilikuwa imetengewa waliojaliwa mali na serikali ikasema hapana. Fedha zilizokuwa zikitozwa zilikuwa zikiingia mifukoni mwa watu binafsi,” akasema Bw Machogu.

Alihoji kuwa, licha ya serikali kuwa ikijitolea kufadhili ununuzi wa vitabu vya kusoma, taasisi za elimu zilikuwa zikikosa bidhaa hizo muhimu.

Alisema kuwa serikali itaendelea kuzisaidia shule na wanafunzi kupitia kutoa mgao wa fedha, sehemu ya jukumu la serikali likiwa kutoa elimu ya hali ya juu, ya bure iliyo lazima kwa kila mtoto.

Alieleza kuwa kuanzia manmo 2003. Serikali ilikuwa imetekeleza elimu ya msingi isiyo na malipo.

Kwa sasa kila mwanafunzi analipiwa Sh1,420 kwa shule za msingi.

Kwa shule za sekondari ya msingi serikali hutoa ufadhili wa kifedha wa Sh15,042 kwa kila mwanafunzi. Wanafunzi wa shule za sekondari hufadhiliwa Sh22,240 kwa kila mwanafunzi.

  • Tags

You can share this post!

Kampuni ya mradi wa kupunguza gesi ukaa yamulikwa kwa...

Utafunaji miraa na michanganyiko ya ‘chewing gum’...

T L