• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 5:50 AM
Serikali yatenga Sh450m kukabili ukame

Serikali yatenga Sh450m kukabili ukame

Na OSCAR KAKAI

SERIKALI imetenga Sh450 milioni kununua mifugo kutoka kwa wafugaji wanaotoka katika Kaunti zilizoathiriwa na ukame. Katibu katika Wizara ya Utumishi wa Umma, Jinsia, Masuala ya wazee na Mipango Maalum, Micah Powon alisema mifugo wanaonunuliwa chini ya mpango huo inatarajiwa kutoa msaada wa chakula kwa familia zilizoathiriwa na njaa.

Kadhalika, mpango huo pia itasaidia kupunguza mzigo kwa wafugaji wa kutafuta maji na malisho.Mpango huo utawafaidi Wakenya zaidi ya 2.1 milioni kutoka Kaunti 23 walioathiriwa na ukame.Akizungumza na wanahabari katika eneo la Pser, Bw Powon alisema kando na pesa hizo zilizotengwa kuwaokoa wafugaji dhidi ya hasara, serikali pia imetenga Sh2 bilioni kukabiliana na njaa na kuepusha maafa ya kibinadamu.

“Kati ya hizo Sh2 bilioni, Sh350 milioni zilienda kwa Wizara ya Maji,na Sh450 milioni kupelekwa kwa Tume ya Nyamanchini (KMC) kununua wanyama dhaifu na waliodhoofika kwa ajili ya kuchinjwa” akasema Bw Powon.Alisema kuwa ununuzi wa mifugo, utawawezesha wafugaji kuepuka hasara na hata wataweza kuzitumia pesa hizo kujikimu na familia yao.

Mpango huo utatekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Msalaba Mwekundu na KMC.Hata hivyo, BwPowon alitoa wito kwa wafugaji kukumbatia mpango huo ili waweze kuiuza mifugo yao kabla ya kufa.Kadhalika, alisema kuwa serikali inaendelea na mpango wa usambazaji wa chakula kwa watu walio katika mazingira magumu.

Waathiriwa wa njaa wanapewa vyakula vya aina mbalimbali huku wengine wakipewa pesa ukame unapoendelea.“Serikali inajitahidi kadiri iwezavyo kupunguza athari za ukame kwa kukusanya rasilimali zote zinazoweza kutumika,” akasema Bw Powon.Alisema lengo ni kuendelea kupunguza umaskini na njaa kwa watu wanaotoka katika maeneo ya ukame.

  • Tags

You can share this post!

Ngamia, mnyama ambaye manufaa yake hayakadiriki

Wakazi mjini Moi’s Bridge sasa wapumua

T L