• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 10:50 AM
Uhuru asisitiza umuhimu wa umoja

Uhuru asisitiza umuhimu wa umoja

PSCU na CHARLES WASONGA

RAIS Uhuru Kenyatta Jumapili alikariri umuhimu wa umoja wa kitaifa alipoongoza taifa katika sherehe ya maadhimisho ya Jamhuri Dei katika bustani ya Jamhuri, Nairobi.

Bustani hiyo ilikarabatiwa na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) kutokana na umuhimu wake kihistaria kwani hapo ndipo bendera ya mkoloni ilishushwa na bendera Kenya ikapandishwa ili kuipa Kenya uhuru mnamo 1963. Akiongea katika hafla hiyo Rais Kenyatta alisema Kenya inaweza tu kufikia maendeleo ikiwa wananchi wote watafanya kazi pamoja.

Alisema Kenya ni zao la ushirikiano na hakuna mtu au kundi la watu ambao wanaweza kulijenga bila kuhusisha Wakenya wengine, akisema mchango wa kila mmoja ni muhimu. “Tunajenga nyumba moja inayoitwa Kenya na hakuna nafasi kwa ubinafsi katika mradi huu.

Ni kazi ya pamoja ya kila Mkenya mwenye uwezo. Kweli tunaweza kutofautiana wakati mwingine lakini katika kutofautiana kwetu, sharti tuendelee kuheshimiana. “Kwa hakika, kutofautiana kwa njia ya heshima ndio huchangia maridhiano. Kwa hakika tunaweza tu kufikia maendeleo ikiwa tunatofautia,” Rais Kenyatta akasema.

Naibu Rais William Ruto na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga pia waliongea katika hafla hiyo ya kitaifa iliyoadhimishwa kwa maombi, nyimbo, densi na miondoko ya wanajeshi. Dkt Ruto alimpongeza Rais Kenyatta kwa kuongoza mpango wa ukarabati wa bustani ya Uhuru na kuigeuza kuwa eneo maridadi, akisema daima Wakenya watamkumbuka rais kwa hili.

“Kwa niaba ya Wakenya wengine waliofika katika bustani hii kwa mara ya kwanza leo, tungependa kukushukuru kwa kujitolea kwako kufanikisha ukarabati wa uwanja huu hadi ukawa kweli, Uhuru Gardens,” akasema Dkt Ruto. Kwa upande wake Bw Odinga alikubaliana na Rais Kenyatta kuhusu umuhimu wa kutunza bustani hiyo kutokana na umuhimu wake wa kihistoria.

“Kuna wale wanaosema tunapaswa kusahau yaliyopita na tunafaa kulenga yajayo. Yaliyopita ni muhimu kwa sababu tusipoyakumbuka tunaweza kurudia makosa ya zamani,” Bw Odinga akasema. Wengine waliohudhuria sherehe hiyo ya kuadhimisha miaaka 57 tangu Kenya ilipotangazwa kuwa Jamhuri mnamo Desemba 12, 1964 walikuwa kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi na mawaziri kadhaa.

You can share this post!

Wiper yajitenga na Gideon Moi kuhusu kuunga Raila 2022

Hofu vimbunga vikiua watu 100

T L