• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Ari yenu isiishe nari, Uhuru awashauri wanajeshi wapya

Ari yenu isiishe nari, Uhuru awashauri wanajeshi wapya

PSCU na CHARLES WASONGA

RAIS Uhuru Kenyatta ametoa changamoto kwa wanajeshi wapya waliofuzu kutoa huduma kwa weledi ambao umekuwa ukidhihirishwa na jeshi la ulinzi la Kenya (KDF).

Akiongea katika sherehe za kufuzu kwa makurutu wa KDF katika chuo cha mafunzo ya makurutu viungani mwa mji wa Eldoret, Rais Kenyatta alishauri wanajeshi hao kuwa kielelezo chema ndani na nje ya kambi zao.

“Leo mnapojiunga na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), mkumbuke kuwa jeshi letu linaheshimiwa na kupendwa katika eneo hili na ulimwengu kwa ujumla. Wanajeshi wetu hudhihirisha uaminifu, uzalendo na fahari ya Wakenya,” Rais Kenyatta akasema.

“Kwa hivyo, sharti mtekelezea majukumu yenu kwa nidhamu kwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazoongoza utendakazi wenu. Katika kila kitu mnayofanya mkiwa kazini au mapumzikoni, muonyeshe sifa za mwanajeshi,” kiongozi wa taifa akaongeza.

Huku akiwapongeza wanajeshi hao waliofuzu, Rais Kenyatta alisema wamefuzu wakati muhimu ambapo Kenya inakabiliwa na tishio la uvamizi kutoka nje.

“Mnajiunga na vikosi vya wanajeshi wetu wakati ambapo uhuru wetu na maeneo yetu ya mipaka ardhini na majini unakabiliwa na vitisho,” Rais Kenyatta akasema.

Kenya imetofautiana na taifa jirani la Somalia kuhusu eneo la mpaka wa majini katika Bahari Hindi.

Hii ni licha ya Mahakama ya Kimataifa kuhusu Haki (ICJ) kuamua kuwa Somali inafaa kumiliki sehemu kubwa ya eneo hilo linalozozaniwa.

You can share this post!

Raila atarajiwa Nyandarua kwa kampeni kali

Kipa Steffen arefusha mkataba wake kambini mwa Man-City...

T L