• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:32 PM
Raila atarajiwa Nyandarua kwa kampeni kali

Raila atarajiwa Nyandarua kwa kampeni kali

Na CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa ODM Raila Odinga anatarajiwa kuhutubia msururu wa mikutano 10 katika eneo la Mlima Kenya kuanzia Jumamosi, Novemba 6, 2021 baada ya kurejea nchini kutoka Dubai.

Kupitia taarifa iliyotolewa Ijumaa na uongozi wa chama hicho cha Chungwa mnamo Ijumaa, Waziri huyo mkuu wa zamani ataanza ziara yake katika Kaunti ya Nyandarau kusaka uungwaji mkono katika azma yake ya kuwa rais 2022.

Kulingana na ratiba ya kampeni hiyo, msafara wa Bw Odinga utapitia maeneo ya Fly Over, Kwa Haraka, Njabini hadi vijiji vya kikoloni ambako atahutubia wafuasi wake.

“Mheshimiwa Odinga ataandamana na viongozi wa eneo la Mlima Kenya wakiongozwa na mwenyeji wake, Gavana Francis Kimemiah. Vile vile, kutakuwepo na magavana kutoka kaunti za Mlima Kenya, wabunge kadha na madiwani,” ikasema taarifa fupi kuhusu ziara hiyo.

Bw Odinga alirejea nchini mnamo Alhamisi jioni kutoka Dubai ambako alihudhuria Kongamano kuhusu Miundomsingi barani Afrika.

Aliandamana na kiranja wa wengi Junet Mohamed na Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.

You can share this post!

‘Mageuzi’ Kemsa yapata pingamizi

Ari yenu isiishe nari, Uhuru awashauri wanajeshi wapya

T L