• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Vijana wahimizwa kutumia kozi zao kujiajiri

Vijana wahimizwa kutumia kozi zao kujiajiri

NA LAWRENCE ONGARO

MAHAFALI wapatao 5, 700 wa chuo Kikuu cha Mount Kenya waliofuzu mwaka huu, 2023 wamehimizwa kutilia maanani ujuzi waliopokea ili kujiajiri badala ya kutegemea nafasi finyu za kazi za serikali ambazo hazipatikani.

Naibu Chansela Prof Deogratius Jaganyi, alisema licha ya masomo, wamepata ujuzi wa kuwa viongozi na kuonesha talanta zao katika uimbaji na masuala ya kitamaduni.

“Nyinyi kwa wakati huu mumeanza safari ya kupambana na hali ya ulimwengu na hivyo hakuna sababu ya kulalamika,” aliwashauri mahafali hao.

Hafla hiyo ya Ijumaa, Desemba 8, 2023 ilikuwa makala ya 24 kwa mahafali kufuzu katika chuo hicho.

Kauli mbiu ya hafla hiyo ilikuwa “The Role of higher Education in Driving small scale Industry for socio- Economic Equity through Linkage”.

Jaganyi alisema chuo hicho kimeweza kuwapa nafasi wanafunzi wanaosoma  masuala ya kiafya, kusafiri nchi za nje kama vile Uhispanoa, Ufaransa, na Italia ili kujionea mageni.

Alisema cha muhimu zaidi wakati huu ni chuo hicho kuangazia masuala ya utafiti na ubunifu, kwa sababu yanaambatana na jinsi mambo yanavyobadilika maishani.

Mgeni wa heshima katika hafla hiyo alikuwa Katibu wa masuala ya viwanda, biashara na uwekezaji, Dkt Juma Mukhwana aliyesifia sekta ya biashara katika kubuni kiwango kikubwa chaajira nchini.

Aidha, sekta ya biashara ndogo ndogo na zile za kadri (MSMEs), inakadiriwa kuajiri watu wapatao 14.1 milioni ambao wanawakilisha asilimia 93.

Alisema serikali itaendelea kuwapa motisha vijana ili waendelee kujihusisha na biashara ndogo ndogo kwa minajili ya manufaa yao kimaisha.

Wakati wa hafla hiyo wanafunzi kutoka nchi 40 walijumuika na wa hapa nchini kufuzu kupokea shahada mbalimbali za kozi.

Pro-Chansela wa Mount Kenya, Dkt Vincent Gaitho, alisema chuo hicho kinawapa wanfunzi wake ujuzi wa kujitegemea kupitia taaluma zinazohamasisha ubunifu.

“Iwapo umepata maarifa masomoni, jukumu lako sasa ni kuanza kazi mradi tu upate fedha za kujikwamua,” alishauri Dkt Gaitho.

Alisema tayari Mount Kenya imezindua mfumo wa masomo ya mbali kwa njia ya kielektroniki, ndio Open Distance Eletronic Learning (ODEL) ili wanafunzi wenye kiu cha masomo wapate fursa kusoma.

 

  • Tags

You can share this post!

Makahaba wapandisha bei wakilalamikia polisi na Mungiki...

El Nino: Uhaba wa mafuta Lamu kina mama wajawazito...

T L