• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Makahaba wapandisha bei wakilalamikia polisi na Mungiki kuwawekea ushuru

Makahaba wapandisha bei wakilalamikia polisi na Mungiki kuwawekea ushuru

NA MWANGI MUIRURI 

MAKAHABA katika mtaa wa Githurai 45, mpakani mwa Kiambu na Nairobi Desemba 6, 2023 walitangaza nyongeza ya bei ya huduma kwa kati ya Sh50 na Sh100.

Walisema nyongeza hiyo imetokana na hongo ya polisi ambayo imeongezeka kutoka Sh10 kwa kila kahaba kila siku hadi Sh20, huku nalo genge la Mungiki likiongeza ada zake kutoka Sh20 hadi Sh30.

Polisi na Mungiki wamesemwa kuongeza ada zao za ufisadi na ujambazi mtawalia, wakuu wao wakisingizia kupanda kwa gharama ya maisha.

“Katika hali hii, ile huduma ya bei ya chini ya Sh150 sasa imepanda hadi Sh200, ile ya walio na shida ya kumaliza haja yao kwa haraka iliyokuwa Sh200 sasa ikipanda hadi Sh300,” akasema mshirikishi wa makahaba hao katika viunga vya soko la mawe Bi Esther Kahiga.

Huku bei ya usiku kucha ikiwa awali katika kiwango cha chini cha Sh1, 000, kwa sasa mteja wa kawaida atakuwa analipa Sh1, 100 kama bei ya chini.

Wale ambao makahaba huwasifu kama wakarimu na walio na utu wa kupenda maendeleo kupitia kulipa pesa nyingi bila kuzingatia viwango vya bei wataendelea kutunzwa tu kama awali.

Bi Kahiga alisema kwamba “kwa sasa tunashindwa kuelewa polisi na Mungiki wanataka kutufanyia kazi iwe ngumu kwa nini kwa sababu hata wateja wetu wamezidiwa na hali ngumu ya maisha”.

Makahaba hao walisema Mungiki ni afadhali kwa kuwa huwa wanawakinga dhidi ya kupigwa na kuibiwa na wateja wabishi “lakini hawa polisi wa Kasarani huwa wanatuitisha pesa za bwerere”.

Walisema kwamba “hao polisi hasa hutuma maafisa wa kike ambao kando na kujifanya wenzetu, hutekeleza ujasusi wa kutuhesabu ili wajue hongo ambayo itawafikia kama kikosi”.

Ajabu ni kwamba, inaripotiwa kwamba kuna maafisa ambao hujisahau walikuwa wameingia kutangamana nasi ili kutuchunguza na wanaishia pia kunyakua za wateja wa ngono baada ya kugundua ni nyingi kuliko mshahara wa serikali.

“Kwa siku, ikiwa unajua kuoga na kuongea vizuri unaweza ukafanikiwa kupata wateja 20. Kwa kila mmoja akikupa Sh150 utapata hizo ni Sh3, 000 kwa siku. Kwa mwezi hizo ni Sh90, 000. Tuseme hata biashara ni mbaya kiasi gani, kwa mwezi hutakosa zako Sh50, 000,” akasema mmoja wa makahaba.

Hesabu hiyo ndiyo huvutia maafisa wa polisi kuitoza ushuru haramu, huku nao Mungiki wakipata mwanya wa kuvuna kwa kujipanga kama maafisa kienyeji wa usalama kwa makahaba hao.

Sasa, wateja wa ngono wameelezewa kwamba watakumbana na nyongeza ya huduma, makahaba wakijiepusha na lawama na kulimbikizia polisi na Mungiki kashfa hiyo.

“Kuna wateja wazuri ambao hata hawazingatii bei zetu hapa. Kuna mteja hata anaweza akakupa Sh2, 000 kwa huduma ya ‘shot‘ ambayo ndiyo ya bei rahisi. Kunao hata watakupa Sh5, 000 kwa huduma zingine ambazo kwa sasa acha tusiziseme hapa…Hao tunawaenzi sana. Lakini wateja wa kawaida itabidi sasa wapate nyongeza hiyo ya huduma,” akasema Bi Kahiga.

 

  • Tags

You can share this post!

Shinikizo maspika wa mabunge yote wawe na digrii

Vijana wahimizwa kutumia kozi zao kujiajiri

T L