• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 6:50 AM
Wabunge washangazwa na ununuzi wa stima kutoka Rerec

Wabunge washangazwa na ununuzi wa stima kutoka Rerec

Na RICHARD MUNGUTI

WABUNGE jana walishtushwa na ufichuzi kwamba kampuni ya Kenya Power inanunua umeme kutoka kwa shirika la serikali la kusambaza kawi mashambani (Rerec) kwa sarafu ya Dola za Amerika.

Rerec inalaumiwa kwa kujihusisha na uzalishaji kinyume na mwongozo wake.

Ufichuzi huu uligunduliwa na kutambuliwa wakati wa kuchunguza sababu za gharama ya juu ya stima na kamati ya Seneti ya Kawi.

Afisa mkuu wa Rerec Peter Mbugua aliyefika mbele ya kamati hiyo alisema shirika hilo linauzia KPLC megawati 54.65 za umeme unaotengenezwa katika kiwanda cha Garissa Solar Power (GSP).

Bw Mbugua alisema GSP huuzia KPLC stima kwa bei ya Sh7.4 na kwamba itaendelea kuuzia Kenya Power stima kwa muda wa miaka 20 ijayo.

Mkuu huyo wa Rerec alisema GSP ilianza kuuzia KPLC stima Novemba 2018, na kwamba inaidai KPLC Sh600 milioni.

“Tunailipisha KPLC stima hii kwa sababu GSP inalipa mkopo uliofadhili ujenzi wa kiwanda hiki kinachodhibitiwa na KenGen,” Bw Mbugua aliambia wabunge.

Kulingana na mkataba uliotiwa saini 2015, GSP ilistawisha mradi huo kwa Sh10 bilioni.

Aidha, ilepewa muda wa miaka saba ianze kulipa mkopo huo.

Kufikia Julai 2023 muda wa bakshishi uliopewa GSP utayoyoma.

Mkopo huo utalipwa kwa awamu 26.

Afisa huyo alieleleza kamati hiyo kwamba pesa zinazolipwa stima na KPLC zimewekwa katika akaunti maaalum na kufikia sasa kima cha Sh2 bilioni zimekusanywa.

Pesa hizi zitatumika kulipa mkopo huo uliofadhiliwa KenGen na Benki ya China Exim.

Hata hivyo, Bw Mbugua alikabiliwa na wakati mgumu kumweleza Seneta wa Naironi Edwin Sifuna sababu  za GSP kuuzia KPLC stima kwa dola za Amerika ilhali mkopo huo ulifadhiliwa kwa sarafu za Uchina –Yuan.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Mke wa Naibu Rais alia serikali kutaka kudhibiti makanisa

Askofu alalamikia kulazimishwa kubeba kinyesi akiwa seli...

T L