• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Washukiwa wanne wa mtandao wa wizi wa simu wakamatwa jijini Nairobi

Washukiwa wanne wa mtandao wa wizi wa simu wakamatwa jijini Nairobi

NA LABAAN SHABAAN

MAKACHERO wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wamewakamata washukiwa wanne wanaohusishwa na mtandao wa wizi wa simu jijini Nairobi.

Malumasi Aisha na Agaba Anestus Majuni, wote kutoka nchi jirani ya Uganda, walitiwa mbaroni pamoja na Wakenya Sarah Njeri na dada yake Mary Wangui.

DCI inasema ilipata habari za kijasusi na kuwafumania washukiwa hawa katikati mwa jiji la Nairobi wakiendeleza biashara ya simu za wizi.

Wa kwanza kushikwa alikuwa Malumasi akiwa na simu 13 ambazo inaaminiwa zilipangwa kuuzwa nchini Uganda.

Malumasi aliwapeleka wapelelezi hadi katika duka moja lililoko katika kituo cha biashara cha Munyu.

Hapo aliwafichua washukiwa wenzake – Wangari na Wangui – waliokuwa wanapokea simu zaidi zilizoibwa.

Walipofumaniwa na kutiwa nguvuni, washukiwa hao waliandamana na kuwezesha utambuzi wa Majuni.

Wakati huo, raia huyo wa Uganda alikuwa anajiandaa kusambaza simu kusafirishwa hadi nchini mwao akiwa katika kituo cha mabasi ya Simba Coach.

“Tumepanua neti ya kunasa washukiwa zaidi wanaoiba simu ili kuuza katika nchi jirani,” DCI ilisema kupitia mtandao wa kijamii wa X (awali Twitter).

DCI inasema itaendelea kutumia teknolojia ya kisasa kudhibiti na kuvunja mitandao ya wizi wa simu.

  • Tags

You can share this post!

Raila Odinga alivyofurushwa Turkana, MCA akimchemkia kwa...

AMINI USIAMINI: Kuna ndege mchinjaji

T L