• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:50 AM
Watishia kususia uchaguzi mkuu mwaka 2022 kiwanda cha miwa cha Mumias kisipofufuliwa

Watishia kususia uchaguzi mkuu mwaka 2022 kiwanda cha miwa cha Mumias kisipofufuliwa

Na SHABAN MAKOKHA

WAKULIMA, wafanyabiashara na wakazi wa Mumias wanaotegemea uzalishaji wa miwa, wametishia kutoshiriki katika uchaguzi ujao iwapo Kampuni ya Sukari ya Mumias (MSC) haitakuwa imefufuliwa.

Kundi la wakulima, wafanyabiashara, vikundi vya wanawake na wafanyakazi wa zamani wa kiwanda hicho kilichoporomoka, wamemuomba Rais Uhuru Kenyatta na mshirika wake katika handisheki, Raila Odinga kuingilia kati mchakato wa kufufua kiwanda hicho ili kifanye kazi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

“Rais anatutaka tuweke kura zetu katika kapu fulani katika uchaguzi mkuu ujao lakini hatusaidii kufufua uchumi wetu. Hatutamuunga mkono iwapo MSC haitakuwa ikifanya kazi. Kama anaweza kuingilia kati Mumias ianze kufanya kazi, tutakuwa mabalozi wake kuhakikisha maagizo yake yote yanatimizwa,” alisema Bi Refa Odanga, mkazi wa Shibale.

Pia walimwomba Rais Kenyatta kuwasamehe iwapo walimkosea kwa njia yoyote akiwa rais na akome kupuuza matatizo ya eneo la Magharibi.

“Kama tulikukosea au mmoja wa wana wetu alikukosea, tafadhali tusamehe na ujue utuokoe kwa kuwa kwa kweli tunateseka. Tusaidie kufufua Mumias- tegemeo la uchumi wetu,” aliomba Bw Odanga.

You can share this post!

Matiang’i ausifu ukumbi wa kisasa wa Mwai Kibaki...

Ghulamu mtukutu apiganisha wazazi

T L