• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Yafichuka ulaghai wa bima hupotezea serikali mamilioni

Yafichuka ulaghai wa bima hupotezea serikali mamilioni

NA EVANS JAOLA

SERIKALI ya Kenya inapoteza mamilioni ya pesa katika ulaghai wa bima ghushi za magari unaohusisha maajenti wa kampuni zinazotoa huduma, upelelezi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Udanganyifu wa Bima (IFIU) na Chama cha kampuni za Bima Kenya (AKI) umefichua.

Bw Linus Ogwango, Mkuu wa IFIU, alisema kuwa baadhi ya madereva kote nchini wanatumia vyeti ghushi vya bima bila kujua, ulaghai ambao unainyima serikali mapato.

Akizungumza mjini Kitale, Kaunti ya Trans Nzoia wakati wa zoezi la siku mbili la ukaguzi wa magari, lililoendeshwa kwa pamoja na IFIU na AKI, Ogwango alisema waligundua magari kadhaa yalikuwa yakitumia vyeti ghushi vya bima.

Bw Ogwango, ambaye ni kamishna wa polisi, alibainisha kuwa baadhi ya madereva wa magari hawakujua kuwa bima walizokuwa wakitumia ni ghushi ama kutoka kwa kampuni za bima zilizosajiliwa au kampuni ambazo hazipo.

  • Tags

You can share this post!

Pasta asitisha injili kutimua jombi aliyesumbua akihubiri

Pochettino adai Chelsea sasa imeiva kutambisha Carabao

T L