• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Besigye kizimbani tena kwa kuchochea maandamano ya raia

Besigye kizimbani tena kwa kuchochea maandamano ya raia

DAILY MONITOR na AFP

KAMPALA, UGANDA

MWANASIASA mkongwe nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye, ameshtakiwa kwa mara ya pili kwa tuhuma za kuchochea maandamano ya kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha nchini humo.

Hii ni baada ya kuachiliwa kwa dhamana wiki moja iliyopita baada ya kukamatwa kwa makosa yayo hayo.

Besigye, 66, ambaye amekuwa mkosoaji wa Rais Yoweri Museveni kwa miaka mingi, amekuwa akiwaongoza raia kuandamana kupinga kupanda kwa bei ya bidhaa za kimsingi, kufuatia vita nchini Ukraine.

Alikamatwa Jumanne jioni jijini Kampala akiongoza maandamano hayo na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Nagalama kwenye kitongoji cha Mukono.

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Mahamaka ya Buganda Road kumweka rumande katika kipindi cha mwezi mmoja, kwa makosa sawa na hayo.

Mwanasiasa huyo wa upinzani, ambaye amewahi kuwania urais mara nne, alifunguliwa mashtaka mengine Alhamisi kwa kosa la kuitisha maandamano yaliyodaiwa kusababisha uharibifu wa mali.

Maafisa wa polisi walizingira mahakama ya kijeshi ya Buganda Road huku wananchi wakisubiri kumwona Dkt Besigye akiwasilishwa kortini.

Kabla ya shughuli za mahakama kuanza mwendo wa saa kumi na moja jioni, maafisa wa usalama waliweka vituo kadhaa vya ukaguzi wa magari, na watu, katika barabara za kuelekea mahakama hiyo.

Watu walikuwa wakizuia kuingia ndani ya majengo ya mahakama hiyo iliyowekwa chini ya ulinzi mkali.Mwendo wa sasa kumi na moja na dakika 30, maafisa wa usalama waliovalia kiraia, wabunge kadha, mawakili na maafisa wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC) walikuwa wameketi kortini wakisubiri hakimu kusoma mashtaka dhidi ya Besigye na Bw Samuel Lubega Mukaku.

Bw Lubega pia amewahi kuwania urais nchini Uganda. Hakimu Asuman Huhumuza aliingia saa kumi na moja na dakika 56 na kuanza kusoma mashtaka kwa washukiwa.

“Mahakama iliambiwa kuwa mnamo Juni 14, 2022, katika eneo la Nakivubo katikati mwa jiji kuu Kampala, Besigye alichochea maandamano na kuchangia uharibifu wa mali,” Bw Muhumuza akasoma.

Hakimu huyo alikataa ombi la dhamana kutoka kwa mawakili wa washtakiwa, akisema muda wa kuendesha shughuli za mahakama uliokuwa umepita.

Hatua hiyo ilikasirisha wafuasi na mawakili wa viongozi hao wakiongozwa na Erias Lukwago.

Hata hivyo, shinikizo zao ziliambulia patupu kwani hakimu aliamuru washukiwa wazuiliwe katika gereza la Luzira.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Mtindo wa serikali kuchelea kufadhili timu za...

Sonko amejikaanga, IEBC yaambia korti

T L