• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 11:39 AM
Chanjo ya monkeypox ije Afrika – Wanasayansi

Chanjo ya monkeypox ije Afrika – Wanasayansi

NA MASHIRIKA

DRC, CONGO

WANASAYANSI wanaiomba Jumuia ya Kimataifa kusambaza chanjo ya ugonjwa wa ndui ya nyani (monkeypox) Afrika.

Haya yanajiri huku idadi ya maambukizi ya ugonjwa huo yakiendelea kushuhudiwa Barani Afrika.

Wataalamu hao wanasema kuwa kuna haja chanjo dhidi ya ndui hiyo kusambazwa haraka Afrika ili kudhibiti ugonjwa huo kabla wananchi kulemewa.

Mwezi Julai, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliorodhesha ndui ya nyani kuwa janga la kimataifa na kuomba Jumuia ya kimataifa kusaidia mataifa ya kiafrika ili kuepuka ukosefu wa chanjo dhidi yake kama ilivyoshuhudiwa wakati wa janga la corona.

Haya yanajiri miezi michache baada ya visa 1,400 vya ndui ya nyani kuripotiwa katika nchi saba za Afrika.

Visa hivyo viliripotiwa katika nchi za Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Liberia, Nigeria, Congo-Brazzaville na Sierra Leone.

Placide Mbala, mmoja wa watafiti wa magonjwa yanayosambazwa na virusi kutoka taasisi ya kimatibabu ya Congo amesema kwamba hakuna lililobadilika kwa kuwa ulimwengu unashugulikia maambukizi ya ndui ya nyani kwenye mataifa ya magharibi.

Kadhalika, alisema kuwa mataifa ya kiafrika ambako ugonjwa huo umekuwa kwa muda mrefu yamekuwa dhaifu ifikapo kwenye masuala ya utafiti, ufuatiliaji, upimaji pamoja na matibabu kwa wagonjwa.

Ugonjwa huo umeambukiza watu kwenye baadhi ya maeneo ya magharibi na kati mwa Afrika tangu miaka ya 70, lakini ulianza kuzungumziwa kwa kina baada ya kuzuka barani Ulaya na Marekani hivi karibuni.

WHO ilisema kwamba itaweka mikakati ya ugawaji wa chanjo ili kuhakikisha mataifa maskini yanazipata pia.

  • Tags

You can share this post!

Joho aahidi hatajitia ujuzi ‘kumwelekeza’ Nassir

WANDERI KAMAU: Gachagua awasamehe wote na kukumbatia...

T L