• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Corona: Uingereza yawaagiza raia kufanyia kazi majumbani

Corona: Uingereza yawaagiza raia kufanyia kazi majumbani

Na MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona, baada ya visa vya virusi aina ya Omicron kuongezeka.

Miongoni mwa masharti hayo ni kufanyia kazi kutoka nyumbani na hitaji la lazima kwa raia yoyote kuwa na vyeti vya kuonyesha wamepata chanjo dhidi ya virusi hivyo. Kwenye kikao na wanahabari, Johnson alisema maambukizi ya aina hiyo ya virusi yanaendelea kuongezeka, “hali ambayo imeongeza idadi ya watu ambao wamelazwa hospitalini.”

“Lazima tuchukue hatua za mapema ili kudhibiti maambukizi ya aina hii mpya ya virusi,” akasema. Uingereza ndilo taifa la kwanza barani Ulaya kuwaagiza raia wake kufanyia kazi kutoka majumbani mwao. Kufikia sasa, taifa hilo limethibitisha visa zaidi ya 10 milioni huku karibu watu 146,000 wakifariki kutokana na virusi hivyo.

Jana, Waziri wa Afya, Sajid Javid, alisema wamethibitisha visa 568 vya virusi vya Omicron. Alisema kuna uwezekano visa hivyo vimekaribia 10,000 ijapokuwa wanaendelea na juhudi za kuwafanyia ukaguzi watu zaidi ili kujua kiwango halisi cha maambukizi.

You can share this post!

Mauaji: Polisi waashiria kukata rufaa

Bifwoli apeperusha bendera ya Kenya vilivyo uogeleaji Uganda

T L