• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
ICC yataka mibabe sita wa vita Sudan wasalimishwe

ICC yataka mibabe sita wa vita Sudan wasalimishwe

Na AFP

MWENDESHA Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa kuhusu uhalifu, ICC, Fatou Bensouda ameirai serikali ya Sudan kuwapeleka mibabe wanne wa kivita wanaodaiwa kushiriki mauaji ya halaiki eneo la Darfur.

Kufikia sasa, mshukiwa mmoja pekee anayedaiwa kushiriki ghasia hizo Ali Kushayb ambaye yupo ICC baada ya kujisalimisha kwa hiari na kuhamishwa hadi ICC mwaka moja uliopita.Washukiwa wengine ni aliyekuwa Rais Omar al Bashir, aliyekuwa kamanda wa kundi la waasi Abdallah Banda na aliyekuwa waziri wa ulinzi, Abdel Raheem Muhammad Hussein.

“Sudan imedhihirisha kwamba serikali ya sasa inatambua haki na inalenga kushirikiana na ICC kuhakikisha washukiwa wa kivita wanakabiliwa kisheria,” akasema Fatou Bensouda wakati wa kikao chake cha mwisho kama Kiongozi wa Mashtaka ya Baraza la Umoja wa Kimataifa (UN) kama kiongozi wa mashtaka.

“Washukiwa wote sasa wapo chini ya serikali ya Sudan na ni vyema wahamishwe hadi ICC ili washtakiwe hasa kutokana na makosa ya mauaji ya halaiki Darfur,” akaongeza.Vita vya miaka mingi kati ya waasi au wapiganiaji na wanajeshi wa serikali wenye makao ya Khartoum, vilichangia vifo vya zaidi ya watu 300,000 na wengine milioni mbili wakahama makwao kukimbilia usalama wao.

Bensouda alitembelea Darfur wiki jana na akasema makovu ya mauaji hayo bado ni wazi huku akisisitiza waliochangia lazima wawajibikie vitendo vyao liwe liwalo.’Ziara yangu ya kihistoria Darfur wiki jana ilinifungua macho kuhusu mauaji hayo na mateso ambayo yangali yanaendelea. Vita hivyo vimeendelea kwa miaka mingi,” akaeleza baraza la UN.

Alisema kwamba, mshukiwa mwingine Ahmad Harun ambaye alikuwa waziri wa zamani wa usalama chini ya utawala wa Rais Omar al Bashir tayari amesema kwamba yupo tayari kujisalimisha na ni jukumu la serikali ya Sudan kumhamisha hadi Hague Uholanzi.

“Kulingana na kanuni za ICC, Sudan ina jukumu la kuhakikisha kwamba inawapeleka washukiwa wa kivita. Haifai kushurutishwa ilhali mshukiwa kama Harun tayari amekubali kujisalimisha,” akaongeza Bensouda.

Kulingana na mkataba wa amani wa eneo la Juba kati ya Sudan na waasi, iliamuliwa kwamba washukiwa ambao walichangia mauaji ya halaiki wanafaa wakabidhiwe ICC ili washtakiwe baada ya uchunguzi kutamatika.

  • Tags

You can share this post!

ICC yataka mibabe sita wa vita Sudan wasalimishwe

euro hiyo…