• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Kagame aweka wazi azma yake ya kuwania tena urais mwakani

Kagame aweka wazi azma yake ya kuwania tena urais mwakani

NA MASHIRIKA

KIGALI, RWANDA

RAIS wa Rwanda Paul Kagame amekiri kuwa atagombea tena urais mwaka 2024.

Kagame, ambaye alichaguliwa kuwa rais mwaka 2000, anastahili kuendelea na wadhifa huo kwa mwongo mwingine baada ya marekebisho ya katiba mwaka 2015 kumruhusu kuendelea kuiongoza nchi hiyo.

Kagame alifichua hayo katika mahojiano na jarida la Pan-African Jeune Afrique mnamo Jumanne.

Alisema hayo alipoulizwa lengo lake katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.

“Nimefurahishwa na imani ambayo watu wangu wameonyesha kwangu. Nitawatumikia daima, kadri niwezavyo. Ndiyo, nitagombea kiti cha urais tena,” Kagame alisema.

Kagame alishinda uchaguzi uliopita wa Agosti 2017 kwa muhula wa miaka saba kwa asilimia 98.63 ya kura, kulingana na tume ya uchaguzi.

Kagame amepata sifa ya kimataifa kwa kusimamia amani na ukuaji wa uchumi tangu mwisho wa mauaji ya halaiki ya 1994, ambapo takriban Watutsi 800,000 wa kabila la Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.

Lakini amekabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kile ambacho mashirika ya haki za binadamu yanasema ni kukandamiza upinzani wa kisiasa na kunyamazisha vyombo huru vya habari.

Hata hivyo, rais huyo amekuwa akipinga tuhuma hizi.

Amerika mwaka 2015 ilikosoa mabadiliko hayo ya katiba, ikisema Kagame anapaswa kuachia kizazi kipya uongozi wa urais.

Katika mahojiano na Jeune Afrique, Kagame alisema hababaishwi na ukosoaji kutoka nchi za Magharibi.

“Watu wanatakiwa kujitegemea na waruhusiwe kujipanga watakavyo,” alisema.

TAFSIRI: WINNIE ONYANDO 

  • Tags

You can share this post!

Mwanamume akiri kuiba simu ya mrembo akijifanya anampigia...

GWIJI WA WIKI: Dkt Timothy Kinoti

T L