• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 6:55 AM
Kigogo wa upinzani kusalia rumande jaji akijiondoa kesini

Kigogo wa upinzani kusalia rumande jaji akijiondoa kesini

Na MASHIRIKA

DAR ES SALAAM, Tanzania

JAJI wa Mahakama Kuu katika Kitengo kinachoshughulikia Makosa ya Kuhujumu Uchumi na Ulaji Rushwa, Tanzania, Elinaza Luvanda, amejiondoa kwenye kesi dhidi ya kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe.

Hatua hiyo ilijiri baada ya Mbowe kusema hana imani kwamba jaji huyo angemtendea haki katika kesi inayomkabili pamoja na washtakiwa wenzake watatu.

Mbowe ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema alikamatwa Julai pamoja na washtakiwa wenzake watatu.

Wanakabiliwa na mashtaka sita ikiwemo kula njama ya kutekeleza mashambulio na kufadhili vitendo vya ugaidi.

Kesi hiyo sasa imeahirishwa hadi wakati mahakama itakapopangiwa Jaji mwingine huku washtakiwa wakiendelea kubaki rumande.

Jaji Luvanda alielekeza nakala za kesi hiyo zirejeshwe kwa msajili wa korti ili zipangiwe jaji mpya.

Mnamo Jumatatu, Mbowe alielezea kutokuwa na imani na Jaji Luvanda saa chache tu baada ya jaji huyo kutupilia mbali mawasilisho mawili baina ya matatu.

“Nikizungumzia pingamizi la kwanza, ni ukweli usiopingika kuwa kesi hii inavuta hisia nyingi ndani ya jamii na itakuwa njema zaidi kama hatua zote za usikilizwaji wa kesi hii zitaonekana na kubaki kuwa vitafanyika kwa haki na weledi bila hisia zozote za uonevu,” alisema Mbowe.

You can share this post!

Serikali yatahadharisha wafugaji kuhamia kaunti jirani bila...

Hisia mseto Zuma akiachiliwa huru kwa msamaha