• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Kioni: Wabunge wa Azimio waliuza uspika bungeni Sh50

Kioni: Wabunge wa Azimio waliuza uspika bungeni Sh50

NA SAMMY WAWERU

KATIBU Mkuu chama cha Jubilee Jeremiah Kioni amedai baadhi ya wabunge Azimio waliuza wadhifa wa spika, anaosema ulipaswa kuwa wa upinzani.

Bw Kioni alisema Jumatatu, Mei 22, 2023 kwamba wabunge hao walihongwa na serikali tawala ya Kenya Kwanza kuuza kiti hicho kwa Sh50 pekee.

Chama hicho kilichoongoza taifa kati ya 2013 – 2022 chini ya uongozi wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, kimefanya Kongamano lake la Kitaifa jijini Nairobi.

“Baadhi ya wabunge wetu Azimio waliuza kiti cha spika wa bunge kwa sababu ya sahani ya chakula,” Kioni alisema akihutubu katika kongamano hilo.

Aliongeza: “Inashangaza kuona waliuza wadhifa huo kwa Sh50 pekee.”

Katibu huyo alidai endapo wabunge wa Azimio wangeungana, muungano huo ungedhibiti kamati zote bungeni.

Alizidi kushikilia kauli ya Azimio kwamba serikali ya Kwanza Kenya inayoongozwa na Rais William Ruto, haikuchaguliwa kihalali.

Wachama wa Jubilee wakati wa Kongamano la chama hicho Nairobi Mei 2023. Picha / LUCY WANJIRU

Kinara wa Azimio Raila Odinga Agosti 2023 alimenyamana na Rais Ruto, japo hakuibuka mshindi.

Kesi yake kupinga kura za ushindi wa Dkt Ruto katika Mahakama ya Juu Zaidi Nchini, hata hivyo, ilifutilia mbali.

“Endapo tungedhibiti kamati zote bungeni, gharama ya juu ya maisha ingeshuka…Ikiwa tungelinda ushindi wetu bungeni, tungeangusha Mswada wa Fedha 2023 unaotarajiwa kugaragazwa bungeni,” Kioni alisema.

Alisema, aliyekuwa spika Kenneth Marende endapo angerejea bungeni angeletea Wakenya afueni kwa sababu bunge ni mojapo ya asasi inayochangia kuamua utendakazi wa serikali.

Jubilee imegubikwa na mgogoro wa uongozi, ikikumbukwa kuwa Bw Kioni aliondolewa kama Katibu Mkuu na nafasi yake kutwaliwa na aliyekuwa mbunge wa Kieni, Bw Kanini Kega.

Bw Kega anaunga mkono utawala wa Rasi Ruto, licha ya 2022 kuwa nyuma ya Odinga.

Rasi mstaafu Uhuru Kenyatta, pia alibanduliwa kama kiongozi na mwenyekiti nafasi yake ikitwaliwa na mbunge maalum Sabina Chege.

  • Tags

You can share this post!

Kongamano la Kitaifa la Jubilee

Raila Odinga katika Kongamano la Kitaifa la Jubilee

T L