• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 12:31 PM
KMJA yaeleza hofu baada ya afisa wa mahakama kuuawa kwa kupigwa risasi

KMJA yaeleza hofu baada ya afisa wa mahakama kuuawa kwa kupigwa risasi

Na RICHARD MUNGUTI

CHAMA cha majaji na mahakimu nchini (KMJA) kimesikitishwa na mauaji ya mfanyakazi wa mahakama ya Migori Phoebe Auma mnamo Ijumaa, Mei 5, 2023.

Bi Auma alipigwa risasi akiwa kwenye pikipiki akielekea kazini.

Alikufa papo hapo.

Dereva wa piki piki hiyo alipata majeraha na amelezwa katika hospitali ya Migori.

Kufuatia kuuawa kwa Bi Auma, rais wa KMJA Bw Derrick Kutto amesema maisha ya maafisa wa idara ya mahakama yamo hatarini.

Bw Kutto aliitaka idara ya uchunguzi wa jinai DCI kuchunguza kwa kina mauaji hayo.

“Tumesikitishwa na mauaji ya Bi Auma akielekea kazini katika mahakama ya Migori mnamo Mei 5, 2023,” alisema Bw Kitto

Bw Kutto alisema kuuawa kwa Bi Auma ni ishara kuwa maisha ya wafanyakazi wa idara ya mahakama yamo hatarini.

“Ikiwa maisha ya makarani wa mahakama yamo hatarini basi maisha ya Majaji na Mahakimu pia yamo hatarini,” Bw Kutto aliambia Taifa Leo kwa njia ya simu jana.

Rais huyo wa KMJA alitoa wito kwa DCI kuchunguza kisa hiki huku akisema “anahofia usalama wa watumishi wa idara ya mahakama.”

“Tunaomba Rais William Ruto atenge wakati akutane na maafisa wa KMJA wamweleze kwa kina masuala kadhaa kuhusu usalama na utenda kazi wao,”

Aliyekuwa hakimu mkuu mahakama ya Mombasa Doreen Mulekyo alivamiwa na majambazi akitoka kazini lakini hawakumjeruhi.

  • Tags

You can share this post!

Gavana Mung’aro amtetea Pasta Ezekiel akidai wamewahi...

Mung’aro aahidi kuboresha huduma za afya mashinani 

T L