• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Gavana Mung’aro amtetea Pasta Ezekiel akidai wamewahi peleka chakula pamoja Shakahola   

Gavana Mung’aro amtetea Pasta Ezekiel akidai wamewahi peleka chakula pamoja Shakahola  

 

NA WINNIE ATIENO

GAVANA wa Kilifi, Bw Gideon Mung’aro, amedai kuwa, mhubiri wa kanisa la New Life, Bw Ezekiel Odero, aliwahi kuzuru Shakahola lakini si kwa sababu yoyote ya kihalifu.

Akimtetea mhubiri huyo anayeandamwa na madai ya mauaji ya halaiki miongoni mwa madai mengine, Bw Mung’aro alisema aliwahi kuandamana naye hadi Shakahola kusambaza vyakula vya msaada.

“Pasta Ezekiel anajulikana na matendo yake yako wazi. Kwa nini ahangaishwe? Amekuwa mstari wa mbele kusaidia watu hasa wahanga wa baa la njaa na hata kulipia wanafunzi karo ya shule,” akasema Bw Mung’aro.

Akizungumza katika Shule ya Msingi ya Mwarakaya Chonyi, Kaunti ya Kilifi, Bw Mung’aro alisema hana wasiwasi wowote kuhusu jinsi anavyozidi kuhusishwa na Bw Odero, akisema yuko tayari kumtetea.

Bw Odero alianza kuchunguzwa baada ya vifo vya halaiki ya watu kugunduliwa katika msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi, ambao wanadaiwa walikuwa waumini wa dhehebu linalohusishwa na mhubiri Paul Mackenzie.

Polisi walidai kuwa, kuna uhusiano kati ya wahubiri hao wawili.

Mahakama ilimwachilia huru Bw Odero wiki iliyopita kwa bondi ya Sh3 milioni au Sh1.5 milioni pesa taslimu, huku akisubiri kufunguliwa mashtaka.

 

  • Tags

You can share this post!

Mfalme Charles III kuongoza nchi 15

KMJA yaeleza hofu baada ya afisa wa mahakama kuuawa kwa...

T L